“Usimtafsiri mtu kutokana na maneno ya watu, ishi nae kwanza ujionee, yote ni kwa sababu binadamu huishi maisha tofauti kulingana na watu tofauti - “ BWM
Richard Steven Itembe - Ricky retweeted
Alama katika kipindi cha majilio.
Taji na mishumaa ya Kipindi cha Majilio. Katika kipindi cha Majilio, tunatafakari alama mbalimbali za kiroho, mojawapo ikiwa ni Taji ya Majilio yenye mishumaa minne. Kila mshumaa unawakilisha juma moja katika kipindi hiki cha maandalizi ya kumpokea Bwana wetu Yesu Kristo.
Mishumaa mitatu huwa ya rangi ya urujuani (purple) na mmoja wa rangi ya waridi (pink). Rangi ya urujuani ni ishara ya toba, majuto na maandalizi ya kiroho. Inatukumbusha kujichunguza, kutubu dhambi zetu na kujiandaa kumpokea Kristo anayekuja. Rangi ya waridi huwakilisha furaha tunapokaribia kusherehekea kuzaliwa kwa Mwokozi wetu. Taji yenye umbo la duara inatukumbusha upendo wa Mungu usio na mwisho kwa wanadamu.Majani mabichi yanayotumika kutengeneza taji hii ni ishara ya uhai na matumaini tunayoyapata kwa njia ya Kristo, ambaye ndiye chanzo cha uzima wetu.
Katika Dominika ya kwanza ya Majilio, tunawasha mshumaa wa kwanza, unaohusishwa na Nabii Isaya. Nabii Isaya alitabiri ujio wa Masiha na kutangaza matumaini kwamba Mungu hajawasahau watu wake, bali atatimiza ahadi yake ya kuwaletea Mwokozi, Emanueli, yaani Mungu pamoja nasi. Mshumaa huu unatualika kuishi katika matumaini na kumtumaini Mungu katika hali zote za maisha yetu.
Dominika ya pili ya Majilio, tunawasha mshumaa wa pili, unaohusishwa na Yohane Mbatizaji. Yohane alikuwa mtangulizi wa Kristo, aliyetumwa kuwaandaa watu kumpokea Masiya. Alikuwa sauti ya anayelia nyikani, akiwaita watu watubu na kuzitengeneza njia za Bwana. Nasi tunaalikwa kuwa watangulizi na watambulishi wa Kristo kwa wengine kwa njia ya maneno na matendo yetu mema.
Katika Dominika ya tatu ya Majilio, inayojulikana kama Gaudete, tunawasha mshumaa wa tatu wenye rangi ya waridi. Rangi hii ni ishara ya furaha kwa sababu tunakaribia kusherehekea kuzaliwa kwa Kristo. Inatukumbusha kwamba safari yetu ya maandalizi inaendelea vizuri na kwamba Bwana yuko karibu nasi. Tunaalikwa kuishi katika furaha, matumaini na amani tunapomsubiri Mwokozi wetu.
Katika Dominika ya nne ya Majilio, tunawasha mshumaa wa nne, unaohusishwa na Bikira Maria na upendo. Mama Bikira Maria alionesha upendo na utii mkubwa kwa Mungu kwa kukubali kuwa sehemu ya mpango wake wa ukombozi wa mwanadamu. Kwa njia yake, Mungu alitimiza ahadi yake ya kumleta Mkombozi wetu, Yesu Kristo. Nasi tunaalikwa kujifunza kutoka kwa Bikira Maria moyo wa unyenyekevu, utii na upendo kwa Mungu.
Ndugu zangu, Mwenyezi Mungu atusaidie katika safari hii ya Majilio ili tunapotafakari alama hizi za kiroho, tusibaki kuzitazama kwa macho tu, bali tuzielewe na kuziishi katika maisha yetu. Tuandae vyema mioyo yetu kwa toba, sala, upendo na matendo mema ili Kristo apate nafasi ya kuzaliwa na kutawala ndani ya mioyo yetu.. 🙏
Richard Steven Itembe - Ricky retweeted
Leo ni dominika ya kwanza ya Kipindi cha Majilio mwaka B wa Kanisa. kwa Dominika hii ya kwanza ya Majilio tunaanza mwaka mpya wa kiliturjia, mwaka B wa Kanisa. Liturujia ya Neno la Mungu ya Dominika hii inatualika, “Kuwa macho, kukesha na kuomba” kwa sababu hatujui siku wala saa atakapokuja tena Bwana wetu Yesu Kristo. Katika kipindi hiki cha Majilio, tumwombe Mungu atujalie neema ya kujiandaa vyema kumpokea Kristo.
Majilio ni nini? Neno Majilio limetokana na neno la Kilatini Adventus, linalomaanisha ujio au kuwasili. Katika Dola ya Kirumi, neno hili lilitumika kuelezea ujio rasmi wa Kaisari au mfalme alipotembelea miji au kurejea kutoka vitani akiwa mshindi. Wananchi walijiandaa kumpokea kwa heshima kubwa kwa kusafisha na kupamba miji, kuandaa maandamano na kufanya sherehe mbalimbali za kumpokea. Baadaye, Wakristo walilipokea neno hili na kulipa maana ya kiimani, likimaanisha ujio wa Mungu duniani katika nafsi ya Mwanaye Yesu Kristo.
Mungu wetu ni Baba mwenye huruma. Anatupenda licha ya madhaifu na dhambi zetu. Baraka tunazopokea kila siku ni ishara ya wema wake. Sisi nasi tunapaswa kujibu upendo huo kwa kumpenda Mungu, kuwapenda wenzetu, kuwasamehe na kuwahurumia kama anavyotuhurumia sisi. Majilio yatukumbushe kuwa Kristo anakuja kwetu kwa sababu anatupenda na tunamhitaji kama Mwokozi wetu.
Ndugu mpendwa, mara nyingi tunamkumbuka Mungu tunapokuwa katika shida, magonjwa na mahangaiko. Lakini tunapopata baraka tunamsahau na wakati mwingine kurudi katika dhambi. Majilio yatufundishe kudumu katika upendo na uaminifu kwa Mungu, si wakati wa shida pekee, bali pia wakati wa mafanikio na raha.
Ndugu zangu, dhambi nazo hututenganisha na Mungu na kutufanya watumwa wa matendo maovu. Chuki, wivu, kiburi, rushwa, uongo na kutokusamehe hudhoofisha maisha yetu ya kiroho. Kwa hiyo, Majilio isiwe maandalizi ya sherehe za Noeli pekee, bali iwe kipindi cha kutubu, kupokea Sakramenti ya Kitubio na kurejesha uhusiano wetu na Mungu. Fundisho la nne: Tumruhusu Mungu atubadilishe kama mfinyanzi anavyoumba vyombo vya udongo.
Tunaalikwa kuwa macho, kukesha na kuomba siku zote. Katika somo hili la Injili Takatifu, Yesu anatukumbusha kwamba hatujui siku wala saa ya ujio wake. Kukesha si kukaa macho usiku bila kulala, bali ni kuwa tayari kiroho, kudumu katika sala na kuishi maisha yanayompendeza Mungu. Ndugu zangu, tusisubiri tupatwe na magonjwa au matatizo ndipo tumkumbuke Mungu. Tuwe na muda wa kusali, kusoma Neno la Mungu, kupokea sakramenti na kuwasaidia maskini na wasiojiweza. Majilio ni kipindi cha kuamka kutoka katika usingizi wa kiroho na kujiandaa kukutana na Bwana.
Majilio ni kipindi cha kuachana na matendo ya giza na kuishi kama watoto wa nuru. Katika maisha ya Kikristo, giza linawakilisha dhambi, chuki, uovu na matendo yasiyompendeza Mungu. Nuru inawakilisha upendo, haki, ukweli na maisha yanayoongozwa na Kristo, ambaye ndiye Nuru ya ulimwengu.
Ndugu zangu, tulipobatizwa tuliahidi kumkataa Shetani na matendo yake yote na kuishi maisha mapya ndani ya Kristo. Hata hivyo, wakati mwingine tunajikuta tukikumbatia chuki badala ya upendo, rushwa badala ya haki na uongo badala ya ukweli. Kwa hiyo, Majilio isiwe kipindi cha kuwasha mishumaa na kupamba nyumba zetu pekee, bali pia kiwe kipindi cha kuwasha nuru ya Kristo ndani ya mioyo yetu. Tuwe watu wa kusamehe, kupendana, kusaidiana na kuwajali wanaoteseka.
Katika dominika hii ya kwanza ya majilio tuombe neema ya kujiandaa vyema katika kumpokea Kristo atakayezaliwa kwetu, na tumruhusu atawale maisha yetu yote. Tumwombe Mungu atukumbushe daima ufupi wa maisha yetu ya hapa duniani ili tuwe daima macho katika kusali na kutenda mema ili atakapokuja tena katika siku na saa tusiyoijua atukute tupo tayari kumlaki na kuingia mbinguni. 🙏
Richard Steven Itembe - Ricky retweeted
New Price🚨
iPhone 18 Pro
256Gb-3,500,000
512Gb-4,100,000
1TB-5,500,000
iPhone 18 Pro Max
256Gb-3,850,000
512Gb-4,500,000
1TB-5,750,000
All colors available
E-sim only
Non-Active with 1yr warranty
☎️0652795468
Richard Steven Itembe - Ricky retweeted
New Price🚨
iPhone 18 Pro
256Gb-3,500,000
512Gb-4,100,000
1TB-5,500,000
iPhone 18 Pro Max
256Gb-3,850,000
512Gb-4,500,000
1TB-5,750,000
All colors available
E-sim only
Non-Active with 1yr warranty
☎️0652795468
Richard Steven Itembe - Ricky retweeted
Learn to disappoint women’s kwenye emergency zao tunza hela yako Kijana
Richard Steven Itembe - Ricky retweeted
Kheri ya Dominika ya mwisho ya mwaka A. Dominika ya Kristo Mfalme. Yesu ndio Mfalme atawala duniani na mbinguni.
Richard Steven Itembe - Ricky retweeted
Maafisa Wanafunzi wakivalishana vyeo baada ya kutunukiwa Kamisheni na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Amiri Jeshi Mkuu, katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli mkoani Arusha tarehe 21 Novemba, 2026.




























