
Award winning TV/Radio Personality | Hosting Amplifaya on CloudsFM |Journalist from Tanzania covering East Africa and beyond | Bookings [email protected]
Joined April 2010
- Tweets157K
- Following476
- Followers3.1M
- Likes2.1K
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es salaam, imeamuru Serikali kuondoa mara moja vizuizi vyote vya upatikanaji wa mtandao wa kijamii wa X, zamani Twitter, baada ya kubaini kuwa hatua ya kuufunga mtandao huo ilikuwa kinyume cha Sheria na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hukumu hiyo yenye kurasa 45, ya Novemba 24, 2026, imesainiwa na Jopo la Majaji watatu, S.M. Maghimbi, E.B. Luvanda na E.Y. Mkwizu, katika shauri la kikatiba namba 2378 la mwaka 2026, lililofunguliwa na Tito Elia Magoti na Kumbusho Dawson Kagine.
Mahakama imebaini kuwa hatua ya kuzuia upatikanaji wa mtandao huo tangu Mei 20, 2025, ilikiuka Ibara za 18, 20(1), 26(1) na 29(1) za Katiba, huku ikisisitiza kuwa hakuna Sheria inayowapa mamlaka wadaiwa kuzuia upatikanaji wa mtandao mzima wa kijamii.
Aidha, Mahakama imefafanua kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) bado ina mamlaka ya kuondoa au kuzuia upatikanaji wa maudhui mahususi yaliyokatazwa kisheria, lakini si kufunga mtandao mzima.
Mahakama imekubali maombi ya walalamikaji na kuagiza vizuizi hivyo viondolewe mara moja, bila kutoa amri kuhusu gharama za shauri kutokana na kuwa lilifunguliwa kwa maslahi ya umma.
#MillardAyoUPDATES
Chagua njia ya malipo uipendayo kati ya kadi, virtual card (OTP) au app ya Mobility pay na ufurahie huduma zetu kwa urahisi. @totalenergies_tz
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia 0800750242.
1
765
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemtaka Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Ayub Rioba Chacha, kuhakikisha taarifa za utekelezaji wa majukumu ya Serikali zinawafikia Wananchi kwa wakati, huku akisisitiza umuhimu wa kujibu kwa haraka hoja na changamoto zinazoibuliwa na Wananchi.
Akizungumza leo, Novemba 27, 2026, katika hafla ya kuwaapisha viongozi wateule Ikulu Jijini Dar es salaam, Rais Samia amesema ameamua kuifanya Idara ya Habari – MAELEZO kuwa kitengo kinachojitegemea ili kuimarisha utendaji wake.
“Tunajibu kwa haraka changamoto za Wananchi, tunajibu kwa haraka mambo yanayolumiwa Serikali, kwa hiyo Kaka yangu, karibu tena Serikalini, nenda kasimamie tena sehemu hii,” amesema Rais Samia.
#MillardAyoUPDATES
1
54
4,417
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemtaka Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, David Silinde kushughulikia migogoro ya ardhi nchini, ikiwemo baina ya Wakulima na Wafungaji, huku akikemea vitendo vya baadhi ya Maofisa Ardhi wasio waaminifu kutoa kiwanja kimoja kwa Watu wawili au watatu.
Akizungumza leo, Novemba 27, 2026, katika hafla ya kuwaapisha viongozi wateule Ikulu Jijini Dar es salaam, Rais Samia ameelekeza kuendelezwa kwa kliniki za ardhi ili kuwafikia Wananchi, kusikiliza changamoto zao na kuzitatua.
Aidha, Rais Samia amehoji sababu za kusuasua kwa miradi ya upimaji wa ardhi nchini licha ya kuanzishwa muda mrefu, akisisitiza kuwa ardhi iliyopimwa inapaswa kuheshimiwa na kutumika kwa mujibu wa matumizi yaliyopangwa.
#MillardAyoUPDATES
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemtaka Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Beng’i Mazana Issa kuhakikisha kunakuwa na mifumo madhubuti ya kudhibiti maudhui yanayokiuka maadili katika mitandao.
Akizungumza leo, Novemba 27, 2026, katika hafla ya kuwaapisha viongozi wateule Ikulu Jijini Dar es salaam, Rais Samia amesema teknolojia na mitandao vina manufaa, lakini pia vina madhara kwa Jamii.
“Ukiuliza TCRA kwa nini mnaachia hizi zisizo na maadili, anasema hatuna vifaa, sasa nendeni mkatazame vifaa gani vinatakiwa, mfumo gani unatakiwa, tufanye nini ili tuweze kuchuja yale yasiyo na maadili, tuyaache yenye maadili yaingie kwa Wananchi,” amesema Rais Samia.
#MillardAyoUPDATES
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekemea matumizi mabaya ya fedha za Serikali yanayofanywa na baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri, akieleza kuwa licha ya Serikali kupeleka fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo, utekelezaji wake umekuwa ukisuasua.
Akizungumza katika hafla ya kuwaapisha Viongozi wateule leo, Novemba 27, 2026, Rais Samia amesema baadhi ya Wakandarasi wamekuwa wakilipwa fedha za awali na kuomba malipo mengine, licha ya utekelezaji wa miradi kutofikia hata asilimia 10.
Aidha, Rais Samia ameitaka TAMISEMI kuhakikisha Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Halmashauri wanawajibika ipasavyo kwa kuwatumikia Wananchi na kutatua changamoto zao, badala ya kusubiri Waziri Mkuu azunguke nchini kufanya majukumu hayo.
“Nataka Waziri Mkuu apumzike, aratibu Serikali hapa, siyo tena kuzunguka kule, mpumzisheni Waziri Mkuu, nendeni kafanyeni kazi zenu,” amesema Rais Samia.
#MillardAyoUPDATES
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemwelekeza Katibu Mkuu Kiongozi kuunda Timu ya Wahandisi kwa ajili ya kupitia makadirio ya gharama za maboresho ya Uwanja wa Benjamin Mkapa, kufuatia mvutano unaokwamisha kuanza kwa kazi hiyo kuelekea mashindano ya AFCON 2027.
Akizungumza leo, Novemba 27, 2026, katika hafla ya kuwaapisha viongozi wateule Ikulu Jijini Dar es salaam, Rais Samia amesema kazi hiyo bado haijaanza kutokana na mshauri elekezi kueleza kuwa makadirio ya gharama ni makubwa.
“Tengeneza timu ya Wahandisi, waangalie hiyo bajeti, kama iko sawa, kazi iendelee, haiko sawa, irekebishwe, kazi iendelee,” amesema Rais Samia.
Rais Samia amesisitiza kuwa Serikali haiwezi kuendelea kuvumilia mvutano huo wakati Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) likisubiri kufanya ukaguzi wa uwanja huo.
#MillardAyoUPDATES
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Novemba 27, 2026, amewaapisha Viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni, wakiwemo Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu, katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam.
Miongoni mwa Viongozi hao ni Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (Waziri wa Mifugo), David Ernest Silinde (Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi), Beng’i Mazana Issa (Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari) pamoja na Cecilia Daniel Paresso (Naibu Waziri wa Kilimo).
Uapisho huo umefanyika siku mbili baada ya Rais Samia kutangaza mabadiliko ya muundo wa baadhi ya Wizara, uteuzi na uhamisho wa Viongozi mbalimbali Serikalini.
#MillardAyoUPDATES
Mtangazaji Edwin Bashiri Sanga maarufu kama Eddo aliyekuwa akiishi na kufanya kazi Mkoani Iringa, amezikwa leo Alhamisi, Novemba 26, 2026 katika makaburi ya familia yaliyopo Mtaa wa Kibwabwa, Kata ya Kitwiru Mkoani Iringa.
Watu mbalimbali wamejitokeza wakati wa mazishi ya Eddo ambaye alifariki dunia Novemba 24 akipatiwa matibabu Hospitalini Makete.
Eddo atakumbukwa kwa uhodari wake Redioni na kwa namna ya kipekee alivyoifanya kazi yake kwa umahiri ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha Wasikilizaji na kusaidia Watu wenye uhitaji.
#PumzikakwaAmaniBingwa #Iringa'sFINEST #SafirisalamaEddo
Rais wa Kenya, William Ruto ametia saini Muswada wa Sheria ya Akina Mama Wanaonyonyesha wa mwaka 2024, na kuufanya kuwa Sheria inayowataka Waajiri kuweka mazingira rafiki kwa Wanawake wanaonyonyesha Watoto wao wanapokuwa kazini.
Kwa mujibu wa Sheria hiyo, Waajiri wanatakiwa kutenga vyumba maalumu, safi na salama kwa ajili ya kunyonyesha au kukamua maziwa, pamoja na kutoa muda wa mapumziko kwa akina Mama ili waweze kutekeleza majukumu yao ya malezi bila kuathiri ajira zao.
Akizungumza katika Ikulu ya Nairobi leo, Novemba 26, 2026, Rais Ruto amesema Sheria hiyo inalenga kulinda haki na utu wa Wanawake wanaonyonyesha, huku akiahidi kutoa maelekezo kwa Watumishi wa Ikulu kuhakikisha taasisi hiyo inakuwa ya kwanza kuweka mazingira yanayofaa kwa akina Mama wanaonyonyesha.
Sheria hiyo pia inakataza ubaguzi dhidi ya Wanawake mahali pa kazi kutokana na ujauzito, kujifungua, kunyonyesha au hali nyingine zinazohusiana na uzazi.
#MillardAyoUPDATES
Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa ameliagiza Shirika la Huduma za Meli Tanzania (TASHICO) kumsimamisha kazi Nahodha wa meli ya New MV Mwanza, Adam Mwisungu kufuatia ajali ya meli hiyo kugonga mwamba wa Bismarck Jijini Mwanza, Novemba 18, 2026.
Akitoa taarifa ya uchunguzi wa ajali hiyo leo, Novemba 26, 2026, Prof. Mbarawa amesema uchunguzi umebaini kuwa ajali hiyo ilisababishwa na makosa ya kibinadamu na si hitilafu za kiufundi, kwani mifumo ya meli hiyo ilikuwa ikifanya kazi vizuri.
Aidha, Serikali imeagiza kufanyika kwa ukaguzi wa mifumo yote ya usalama na uendeshaji wa meli hiyo, pamoja na kuhakikisha wahudumu wake wana uzoefu na umahiri wa kutosha kabla ya kuruhusu kuanza kwa safari rasmi.
#MillardAyoUPDATES
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba amevitaka Vyombo vya Dola kuhakikisha Sheria inachukua mkondo wake katika kushughulikia migogoro ya ardhi baina ya Wakulima na Wafungaji, akisisitiza kuwa hakuna Mtu anayepaswa kujiona yuko juu ya sheria kutokana na uwezo wake wa kifedha au nafasi aliyonayo katika jamii.
Akizungumza akiwa Mkoani Morogoro, Mwigulu amesema “tusifike kwenye mazoea ya kuona Watu kuuana ni jambo la kawaida, mambo haya huwa yanaalika visasi, yanaalika makovu, makovu yasiyopona, hivyo lazima kila Mtu ajue tunaongozwa na Sheria na kila Mtu ajione yuko salama, Sheria inamlinda, siyo pesa yake inamlinda,”.
Aidha, Waziri Mkuu ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufuatilia kesi zote zinazohusu migogoro ya ardhi, Wakulima na Wafungaji, huku akionya kuwa kutosimamia Sheria ipasavyo kunaweza kusababisha Wananchi kujichukulia Sheria mkononi.
#MillardAyoUPDATES
Mwenyekiti wa Kijiji cha Juhudi, Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma, Amos Hussein Kwigira (45), amehukumiwa kifungo cha miaka 40 jela baada ya kupatikana na hatia ya makosa mawili ya rushwa yaliyohusisha fedha za umma kiasi cha shilingi milioni 5.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TAKUKURU Wilaya ya Kakonko, hukumu hiyo imetolewa Novemba 25, 2026, katika Mahakama ya Wilaya ya Kakonko mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Ambilike Japhet Kyamba ambapo Kwigira amekutwa na hatia ya uchepushaji wa fedha na matumizi mabaya ya mamlaka, akihukumiwa miaka 20 jela kwa kila kosa.
Mahakama ilielezwa kuwa mwezi Machi 2026, Kwigira akiwa katika eneo la Kituo cha Mabasi Kakonko, alipokea shilingi milioni 5 kutoka kwa Mfugaji, ambazo zilikuwa mali ya Kijiji cha Juhudi, na kuzitumia kwa manufaa yake binafsi.
#MillardAyoUPDATES
Wasanii wakongwe wa muziki wa Bongo Fleva, wakiongozwa na Madee Ali ambaye ni mratibu wa Tamasha la Miaka 30 ya Bongo Fleva, leo Novemba 26, 2026, wamewasili Kahama mkoani Shinyanga, tayari kwa ajili ya kutoa burudani kesho, Novemba 27, katika Ukumbi wa Malex Hall, kuanzia saa moja usiku.
Madee ameiambia AyoTV kwamba sababu ya kubadilisha Wasanii wanaotumbuiza katika kila tamasha ni kutoa nafasi kwa Wakongwe wengine wenye sifa za kushiriki, ili kila mmoja apate fursa ya kukutana na Mashabiki wake.
Kwa upande mwingine, Madee ameeleza kuguswa na kifo cha Mtangazaji Edwin Bashiri Sanga, maarufu kama Eddo, kutoka mkoani Iringa, ambapo amesema alikuwa na mchango mkubwa katika kuwaunganisha Wasanii mbalimbali kutoka Nyanda za Juu Kusini, huku akiahidi kushirikiana na Wasanii wenzake kufanya jambo maalumu kwa ajili ya kumuenzi Marehemu.
#MillardAyoUPDATES
Kahama, mlimhola? Zaidi ya wakongwe 30 wa Bongo Fleva, wakiongozwa na Madee Ali, wameondoka Jijini Dar es salaam kuelekea Kahama, tayari kuwasha moto wa burudani katika Tamasha la Miaka 30 ya Bongo Fleva, litakalofanyika kesho, Novemba 27, 2026, katika Ukumbi wa Malex Hall, ni Msanii gani unatamani kuimba naye kwa sauti moja?
#MillardAyoUPDATES
1
75
7,203
#MillardAyoMagazeti Tz & Kenya November 26, 2026
instagram.com/p/DgL0jI1kQ1p/…
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Novemba 25, 2026, amemteua David Ernest Silinde kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, kabla ya uteuzi huo, Silinde alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, nafasi ambayo sasa ameteuliwa Cecilia Daniel Paresso.
#MillardAyoUPDATES
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Novemba 25, 2026, amemteua Beng’i Mazana Issa kuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Beng’i Issa anachukua nafasi ya Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki, ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kufuatia mabadiliko ya muundo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, uapisho wa Mawaziri wateule utafanyika katika tarehe itakayopangwa baadaye.
#MillardAyoUPDATES
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Novemba 25, 2026, amemhamisha Gerson Partinus Msigwa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenda kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Novemba 25, 2026 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, nafasi ya Msigwa katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imechukuliwa na Abdallah Hassan Mitawi, ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi.
#MillardAyoUPDATES


















