fm_☄ (@Bioethics_Tz) header
fm_☄ (@Bioethics_Tz) profile picture

I am because we are.

Paris, France
Joined August 2022
Photo by fm_☄ (@Bioethics_Tz)Photo by fm_☄ (@Bioethics_Tz)Photo by fm_☄ (@Bioethics_Tz)Photo by fm_☄ (@Bioethics_Tz)Photo by fm_☄ (@Bioethics_Tz)Photo by fm_☄ (@Bioethics_Tz)Photo by fm_☄ (@Bioethics_Tz)Photo by fm_☄ (@Bioethics_Tz)Photo by fm_☄ (@Bioethics_Tz)Photo by fm_☄ (@Bioethics_Tz)
“Kilele cha kumcha Mwenyezi Mungu ni kuwatendea watu haki kwa kuwapa wanachostahili, hata kama kufanya hivyo kutakulazimu kujinyima au kupunguza haki na maslahi yako mwenyewe.” Haki ya kweli huonekana pale tunapoitanguliza haki ya wengine mbele ya maslahi yetu binafsi.
45
106
2
544
15,361
Mwanafunzi darasa 6 akutwa akiuza icreem saa 8 usiku karia koo.
3
13
55
6,257
My statement on the conviction of Tanzanian opposition leader, Mr Tundu Lissu.
1
332
21
805
36,459
fm_☄ retweeted
Mawakili, Viongozi wa CHADEMA na wadau mbalimbali wamefurika kwenye ukumbi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam tayari kusikiliza hukumu ya kesi ya uhaini inayomkabili rais mstaafu wa TLS, Wakili Tundu Lissu leo Novemba 06, 2026.
2
82
3
416
16,149
fm_☄ retweeted
ALICHOANDIKA WAKILI MWABUKUSI KWA KISWAHILI: Ndugu yangu, Godbless Lema Hakuna aina ya utumwa iliyo bora kuliko nyingine. Mtumwa ni mtumwa, iwe utumwa wa nyumbani au wa mashambani. Kama viongozi, wanamageuzi na wanaharakati wanaoamini katika utofauti, ni lazima tujitayarishe kukubali kukosolewa, iwe unaonyeshwa vyema au hasi. Tofauti zetu katika mikabala tunayotumia katika kupigania demokrasia si udhaifu; badala yake, yanaonyesha ukweli wa mitazamo na viwango vyetu tofauti vya uelewa. Kila mtu ana jukumu la kutekeleza na mchango wake, licha ya mapungufu yaliyomo katika kila moja ya njia zetu. Tofauti zetu za kimkakati, zenyewe, ni sehemu ya ubinadamu wetu. Hata miongoni mwa wanafunzi wa Yesu, kulikuwa na wale ambao walikuwa na mwelekeo zaidi kuelekea uchumba na mawasiliano, kama vile Filipo, wakati wengine, kama Simoni Petro, walikuwa wahafidhina zaidi. Ndiyo maana Wagiriki waliotoka Bethsaida walimwendea Filipo ili awaunganishe na Yesu badala ya kwenda kwa Petro! Kutoelewana na tofauti kati ya wanaharakati wa nyumbani na wale walio ughaibuni lazima kamwe kutufanya tupoteze picha kubwa zaidi. Hatupaswi kupoteza mwelekeo wetu kwa sababu ya tofauti zetu. Vipaumbele vyetu lazima vibaki 1. UHURU NA HAKI KWA TUNDU LISSU. 2.  HAKI KWA WAATHIRIKA WOTE WA KESI ZINAZOCHOCHEWA KISIASA. 3.HAKI KWA WAATHIRIKA WOTE WA DHULMA NA UONEVU KABLA, WAKATI NA BAADA YA UCHAGUZI MKUU WA TAREHE 29 OKTOBA 2025. Mbele ya mapambano haya ya kawaida, ni wapi basi, uhalali wa mapigano haya yote? Ndugu yangu kwa heshima yote inayostahili Hebu tushiriki  kupitia mawazo na mabishano, tukumbatie tofauti zetu, tuheshimiane, na tusiruhusu kutoelewana kibinafsi kutukengeusha kutoka kwa misheni yetu ya pamoja. UKWELI, HAKI NA UWAJIBIKAJI NDIO NJIA PEKEE YA KULIPONYA TAIFA LETU. BAK MWABUKUSI
My Brother, Godbless Lema No form of slavery is better than another. A slave is a slave, whether domestic or plantation slavery. As leaders, reformists and activists who believe in diversity, we must be prepared to accept criticism, whether expressed positively or negatively. Our differences in the approaches we adopt in the struggle for democracy are not a weakness; rather, they reflect the reality of our different perspectives and levels of understanding. Everyone has a role to play and a contribution to make, despite the shortcomings inherent in each of our approaches. Our strategic differences are, in themselves, part of our humanity. Even among the disciples of Jesus, there were those who were more inclined towards engagement and outreach, such as Philip, while others, like Simon Peter, were more conservative. That is why the Greeks who came from Bethsaida approached Philip to connect them with Jesus rather than going to Peter! Disagreements and differences between activists at home and those in the diaspora must never make us lose sight of the bigger picture. We must not lose our direction because of our differences. Our priorities must remain 1. FREEDOM AND JUSTICE FOR TUNDU LISSU. 2.  JUSTICE FOR ALL VICTIMS OF POLITICALLY MOTIVATED CASES. 3.JUSTICE FOR ALL VICTIMS OF INJUSTICE AND OPPRESSION BEFORE, DURING AND AFTER THE GENERAL ELECTION OF 29 OCTOBER 2025. In the face of these common struggles, where, then, is the justification for all this infighting? My brother with all due respect Let us engage  through ideas and arguments, embrace our differences, respect one another, and never allow personal disagreements to distract us from our common mission. TRUTH, JUSTICE AND ACCOUNTABILITY ARE THE ONLY PATH TO HEALING OUR NATION. BAK MWABUKUSI
5
26
118
18,650
fm_☄ retweeted
Pumzika kwa amani mzee wetu. Pole nyingi kwa familia na mwenyekiti wetu huko GEREZANI ulipo.🙏🏾
49
248
6
1,560
33,480
#BREAKING: MWIGIZAJI MAARUFU SIR PATRICK STEWART AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 86 Mwigizaji mashuhuri wa Uingereza, Sir Patrick Stewart, anayejulikana zaidi kwa nafasi zake za Kapteni Jean-Luc Picard katika Star Trek na Profesa Charles Xavier katika filamu za X-Men, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 86 baada ya kuugua kwa muda mfupi ugonjwa wa Alzheimer na Lewy Body Dementia. Stewart alikuwa nguli wa sanaa ya uigizaji aliyedumu jukwaani na kwenye filamu kwa zaidi ya miongo sita, akijijengea heshima kubwa kutoka ukumbi wa michezo wa Royal Shakespeare Company hadi kuwa mmoja wa waigizaji waliotukuka zaidi duniani. Umahiri wake wa kipekee, sauti yake ya kuvutia na mchango wake mkubwa katika filamu, tamthilia na sanaa ya maonesho ulimpatia hadhi ya ushujaa (knighthood) mwaka 2010. Anaacha urithi mkubwa wa kazi za kisanii zilizogusa na kuhamasisha vizazi vya watazamaji duniani kote.
6
23
2,563
Huyu kiumbe amesema ukweli, jinsi MaCCM wanavitumia vyombo vya dola kwa maslahi yao binafsi. Ni uthibitisho ambao waliuficha gizani. Wameamua kufunguka na kusema ukweli. Watanzani wenzangu, lazima upuuzi huu tujibu kwa kiwango cha kutosha. Tusipuuze. MaCCM wanajaribu kutumia uelewa hafifu wa wananchi katika masuala ya katiba, kupotosha. 1.Ibara ya 3(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza kwamba Jamhuri ya Muungano ni nchi ya kidemokrasia yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa. Mamlaka ya chama (CCM), Sheria ya 1984 Na.15, ilitungwa wakati wa chama kimoja, (Ibara ya 10 imefutwa na Sheria Na.4 1992). CCM ni chama cha siasa, siyo dola. CCM siyo mamlaka ya nchi. 2.Ibara ya 4 ya Katiba ya JMT inataja vyombo vinavyotekeleza mamlaka ya nchi: Serikali, Mahakama, Bunge na Baraza la Wawakilishi kwa mujibu wa maeneo yake ya mamlaka. CCM haijawekwa katika Ibara hiyo kama chombo cha mamlaka ya nchi. Hili ni jambo la msingi: chama cha siasa si chombo cha dola kwa sababu tu kinaongoza Serikali. Hii ieleweke vizuri. 3.Ibara ya 8(1) ya katiba ya Tanzania ndiyo inatoa jibu la moja kwa moja zaidi. Katiba inaeleza kwamba: Mamlaka yote kuhusu nchi hutoka kwa wananchi. Na inaendelea kueleza kwamba; Serikali inapata mamlaka yake kutoka kwa wananchi kupitia Katiba ya Jamhuri ya Muungano, lengo kuu la Serikali ni ustawi wa wananchi, na Serikali inawajibika kwa wananchi. 4.Ibara ya 147(2) inasema Serikali ya Jamhuri ya Muungano ndiyo inaweza, kwa mujibu wa sheria, kuunda na kuweka majeshi kwa ajili ya ulinzi na usalama wa nchi na wananchi wa Tanzania. Katiba ya Tanzania haijasema kwa ajili ya CCM. Hapo ndipo kauli hii ya kipumbavu inapogongana moja kwa moja na Katiba. Katiba ya JMT inataja nchi na wananchi; haisemi chama tawala. 5.Ibara ya 147(3) inakataza askari wa vyombo vya ulinzi na usalama kujiunga na chama cha siasa, isipokuwa haki yake ya kupiga kura. Ibara hiyo inawahusu JWTZ, Polisi, Magereza na JKT. Kama vyombo hivyo vingekuwa mali halali ya CCM, kwa nini Katiba inakataza askari kujiunga na chama cha siasa? Hili ni hitaji la kutenganisha taasisi za usalama na ushindani wa vyama. 6.Ibara ya 148 inamtambua Rais akiwa Amiri Jeshi Mkuu, si Mwenyekiti wa CCM wala Katibu wa CCM. Mamlaka hayo yanatokana na nafasi ya kikatiba ya Rais, si uanachama wake katika chama. CCM ni chama cha siasa siyo dola. Serikali ni chombo cha dola. Vyombo vya ulinzi na usalama ni taasisi za kikatiba/kisheria za dola. Rais ana mamlaka ya kikatiba kama Amiri Jeshi Mkuu 7.Ibara ya 20(1) inampa kila mtu uhuru wa kujiunga na chama na Ibara ya 21(1) inampa kila raia haki ya kushiriki katika utawala wa nchi moja kwa moja au kupitia wawakilishi waliochaguliwa. Leo chama A kinaongoza serikali, kesho chama B kinaweza kushinda uchaguzi. JWTZ, Polisi, Magereza na taasisi nyingine za dola haziwezi kubadilika kuwa mali ya chama cha siasa. 8. Katiba haielezi vyombo vya ulinzi na usalama ni mali ya CCM. CCM ni chama cha siasa tu; JWTZ, JKT, Polisi, Magereza ni taasisi za dola. MaCCM acheni kuchanganya chama na Serikali Ibara ya 147(2) inaeleza wazi Serikali ya Jamhuri ya Muungano inaweza kuunda na kudumisha majeshi kwa madhumuni ya “ulinzi na usalama wa eneo na wananchi wa Tanzania.” Hakuna CCM hapo 9.Ibara ya 148 ya Katiba inampa Rais mamlaka ya Amiri Jeshi Mkuu — si kwa kuwa ni mwanachama wa CCM. Kugeuza taasisi za dola kuwa ‘mali ya CCM’ ni kuchanganya chama na dola Kuyaita ‘mali ya CCM’ mamlaka ya Kikatiba ya RAIS ni kupotoka. CCM inaweza kuongoza Serikali; Katiba ya JMT haibadiliki kuwa mali ya CCM, taasisi za dola hazibadiliki kuwa mali za CCM 10.Katika mfumo wa kikatiba wa vyama vingi, uaminifu wa askari unatakiwa kuwa kwa Katiba na nchi, si kwa chama cha siasa. Hilo ndilo linalofanya Ibara ya 147(3) kuwa na maana zaidi hapa Vyombo hivi vimeanzishwa kwa mamlaka ya Serikali kwa mujibu wa sheria kwa ajili ya nchi na wananchi, ndani ya mfumo wa Katiba si mali ya chama cha siasa. Katiba Mpya is a must MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
21
125
3
594
22,608
*MANENO YA MWISHO YA TUNDU LISU, leo:* “Waheshimiwa Majaji miaka 60 iliyopita, kuna mhaini mwingine alifungwa kifungo cha maisha nchini Afrika Kusini, kabla hajahukumiwa alisema maneno yafuatayo ambayo naomba kuyafanya yawe maneno yangu leo, "I have fought against white domination and I have fought against blood domination, and my Lords, it is an ideal I am prepared to die for" Nimepigania haki na demokrasia kwa sehemu kubwa, kuwa na nchi ya demokrasia, imekuwa ni ideal kwa nchi yangu, msimamo huo umenigharimu sana, umeniletea madhira mengi sana, msimamo huo kwa siku zilizobaki kwa maisha yangu ni msimamo ambao nitaendelea kuusimamia, na kama ikibidi kufa ni msimamo ambao nipo tayari kufa. Namalziia kwa neno moja: waheshimiwa majaji, kosa la uhaini halina kosa dogo, halina kosa ambalo ukishindwa kuthibitisha uhaini unahukumu kwa kosa dogo, it is either death sentence or acquittal, hakuna kakosa kadogo kwenye uhaini, waheshimiwa majaji, mzigo ambao mmekabidhiwa mabegani mwenu ni kuamua kama kwa ushahdii huu kuna uhaini, kama mkiona kuna uhaini you should not hesitate to convict and punish me appropriately, do not hesitate, msiogope, kama mtaona kuna uhaini msiogope kunihukumu, kama mkiona hamna uhaini msiogope kuniachia huru. You have God before you, msije mkaletewa maneno kuna kosa dogo, hakuna kosa dogo kwenye uhaini, if the evidence doesn't fit— acquit, huo ni mzigo ambao ni wa kwenu peke yenu waheshimiwa majaji. Nimemaliza” Tundu Antiphas Lissu, September 28, 2026. Mahakama Kuu, Dar.
62
481
21
1,473
62,815
UHAINI, ambalo ni kosa kubwa kuliko yote ndani ya Jamhuri tena dhidi ya Kiongozi mkuu wa Chama cha Siasa nchini, DPP anashindwa kuleta MASHAHIDI MUHIMU wanaopaswa kujua kilichotokea! Hakuna CDF, IGP, DGIS & DCI. DPP ameshindwa kuleta SSH & viongozi wengine wa Kiserikali ili kuthibitisha ni namna gani WAMETISHIKA! Badala yake, DPP analeta dereva bodaboda, wauza machungwa & wengine toka vijiweni ambao hawahusiki kabisa na masuala ya KIUSALAMA ya Nchi. Yaani, DPP ameokoteza tu vijana mitaani ili kutoa ushahidi tena kwa KIFICHO! Lissu akaona isiwe shida, akataka awalete WAHUSIKA wenyewe, wanakamati ya Usalama ya Taifa. Mahakama ikatoa maamuzi KULINDA wanasiasa. CDF & IGP tukaambiwa wako nje ya nchi, Kingai akatii wito lakini kagoma kutoa ushahidi! Binafsi, nina amini, Lissu alijua fika hawa watu watalala mitini, aliwaita kwa kusudi la kuweka MTEGO, wakanasa. Kama Kingai et al wangekuwa wana AKILI ZA KUTOSHA, wangetoa tu ushahidi. Kitendo cha wao 'kutupa taulo' wakidhani wanamkomoa Lissu, ni MISTAKE. Kiufupi wamesaidia UTETEZI wa mtuhumiwa KUIMARIKA zaidi. Unaesoma ujumbe huu, jiulize tu kama hii kesi si ya KISIASA, kwanini mashahidi wote toka Serikalini WAMEGOMA kutoa ushahidi! Watu ambao tulitegemea watakuja kutueleza nini kilitokea. Mwisho, sote kwa pamoja tuseme LISSU HANA HATIA.
26
174
4
490
11,624
fm_☄ retweeted
VIDEO: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema kuanzisha makundi yenye sura ya kufanya kazi za ulinzi na usalama bila kutambuliwa na mamlaka ni kinyume cha sheria. Katambi ameeleza hayo akizungumza na wanahabari leo mara baada ya mkutano uliomhusisha Sheikh Said Mwaipopo aliyekiri kuwa na kundi la Chui Mweusi na Mbwa Mwitu, akieleza kuwa makundi hayo yaliundwa kutokana na dhamira ya kukabiliana na watu waliokuwa wakipanga kuandamana Waziri Katambi amesema Mwaipopo ameeleza kuwa alichukua hatua hiyo kutokana na uchungu aliokuwa nao kama Mtanzania kufuatia matukio yaliyotokea Oktoba 29,2025 lakini amesisitiza kuwa jukumu la kulinda usalama wa nchi na kuchukua hatua dhidi ya wanaokiuka sheria ni la vyombo vya ulinzi na usalama pekee. Katambi amesema katika ufuatiliaji uliofanyika, hakuna rekodi iliyoonesha kuwa Mwaipopo au kundi lake walijeruhi au kumdhuru mtu, na kwamba Mwaipopo alieleza kuwa alikuwa na nia njema. Hata hivyo, Waziri amesema nia njema haiwezi kuhalalisha njia isiyo sahihi, hivyo amemtaka Mwaipopo na makundi mengine yenye nia ya kushiriki katika masuala ya ulinzi na usalama kufanya hivyo kwa kufuata utaratibu unaotambuliwa na Jeshi la Polisi.
108
11
38
88
83,510
TAL anaingia kwenye kiini cha utetezi wake, anaanza kuhoji kama mashahidi wa Jamhuri wanaaminika vya kutosha kuthibitisha nia ya kufanya kosa la uhaini. Hoja yake ya kwanza inalenga mashahidi wa kificho. Kwa mujibu wa maelezo haya, Lissu anasema mashahidi hao waliwahi kuwa watuhumiwa wenyewe, walikamatwa na Polisi, Na baadhi yao walikiri katika maelezo yao kwamba walikuwa wanapanga kufanya vurugu. Anadai pia walipewa chaguo la kuwa mashahidi dhidi yake badala ya kuendelea kushtakiwa. Hapa kuna hoja muhimu ya kisheria, kwamba kukamatwa au hata kukiri kosa hakumaanishi moja kwa moja kwamba mtu hana uwezo wa kuwa shahidi. Uzito wa ushahidi wao hutegemea mazingira ya kukiri, namna maelezo yalivyopatikana, kama kuna inducement au ahadi, consistency ya maelezo yao, na kama ushahidi wao unathibitishwa na ushahidi mwingine huru. Hivyo, hoja ya Lissu kwamba mashahidi hao ni "totally unreliable" bado ni hoja ambayo Mahakama inapaswa kuitathmini, si hitimisho lililokwishaamuliwa. Anakwenda hatua nyingine kali zaidi, anasema ikiwa Polisi waliwakamata watu kwa madai ya kupanga vurugu, wakawaachia bila kuchukua hatua, halafu baadaye wakawa mashahidi wa Jamhuri, Mahakama inapaswa kujiuliza kwa nini waliaminiwa kama mashahidi na kwa nini hawakuchukuliwa hatua kwa tuhuma walizokiri. Kisha Lissu anaunganisha hoja hiyo na matukio ya 29 Oktoba 2025. Anarejea takwimu zinazodaiwa kuwa kwenye ripoti ya Tume ya Jaji Chande kuhusu vifo katika maeneo mbalimbali. Hoja yake si kwamba mashahidi hao ndio waliosababisha vifo hivyo, hilo linahitaji ushahidi tofauti, bali anatumia mazingira hayo kuhoji uamuzi wa Polisi kuwaachia watu waliodaiwa kuwa walikuwa wamepanga kufanya vurugu. Baada ya hapo utetezi unahamia kwenye jambo muhimu zaidi la mens rea, yaani nia inayotakiwa kuthibitishwa kwa kosa linalodaiwa. Lissu anasema hati ya mashtaka inadai kwamba alitengeneza nia ya kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano, na kwamba nia hiyo ilidhihirishwa kupitia maneno aliyotamka katika mkutano wa 3 Aprili 2025. Kwa hiyo swali ambalo sasa analipeleka mbele ya Majaji ni rahisi lakini ni la msingi sana. Kwamba, Ni ushahidi gani unaothibitisha kwamba Lissu alikuwa na nia hiyo ya kutenda kosa la uhaini? Anaanza kuwachambua PW1, PW16 na PW17 pamoja na exhibits alizoomba Mahakamani. PW1 na PW16, kwa maelezo haya, walifikia hitimisho kwamba kulikuwa na "nia ya kutenda uhaini" kutokana na maneno yaliyosemwa kwenye video. Na hapo ndipo Lissu anaweka hoja nyingine muhimu, kuwa kuna tofauti kati ya kusikia kauli na kutafsiri maana yake na kuthibitisha kisheria kwamba mtu alikuwa na nia ya kutenda kosa fulani.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI Part 279 Mhe. Lissu anaendelea kutoa utetezi wake. 1. Walipanga njama za kufanya uhalifu wakati wa Uchaguzi mkuu mwaka jana. Wote walisema hivyo kwa maandishi hawa mashahidi wa siri na maelezo hayo yaliandikwa Polisi. (Kupiga watu, kuchoma vitu) ni wao walisema hayo. Na ushahidi huo uko hapo mko nao. 2. Wote hao isipokuwa PW4 walikamatwa na Polisi kwa kufanya njama hizo kwa kufanya fujo na wote walikamatwa kwa hizo siku nne yaani Tarehe 04 na Tarehe 08 April. Polisi waliwajua na kuwakamata wote within four days. 3. Mashahidi wote hao baada ya kukamatwa na Polisi wali confess. Walikiri kuwa tunapanga kufanya vurugu kwenye Uchaguzi, wakiwa kizimbani walisema kwamba walipanga kufanya uhalifu tena walikiri hivyo kwa maandishi 4. Mashahidi ambao walikamatwa kama watuhumiwa wote waliachiwa ili waendeleee kupanga njama yani unamkamata mtu kwa uhalifu na unamuachia. 5. Wote waliitwa na Polisi PW 16 Amin Mahamba na kuwambia kubalini kuwa mashahidi dhidi ya Tundu Lissu na mkikubali tutawafutia mashitaka. Wahalifu wamekiri mbele ya Polisi, Wakaachiwa na kuwa mashahidi dhidi ya Tundu Lissu. 6. Wahalifu hao self confessed walitoka Dar es salaam na Dar es salaam Oktoba walikufa watu 182 kwa mujibu wa Jaji Chande. PW 10 and PW 11 Walitoka Arusha na Arusha walikufa watu 53 kwa mujibu wa Jaji Chande. PW13 na PW 14 walitokea Mbeya na huko waliuawa watu 80 kwa mujibu wa Jaji CHANDE. (Polisi walikamata watu waliosema wamepanga kufanya uhalifu Oktoba na wakawaachia na hiyo Oktoba ukatokea huo uhalifu watu hao wakiwa uraiani.) Pw 5 na Pw 7 walitokea Songea na Jaji Chande anasema huko nako walikufa watu ila hawakutaja idadi ya waliokufa Songea. PW 16 Amin Mahamba alisema alikuwa kwenye timu ya wapelelezi walioyachunguza mauaji ya Oktoba 29 na nikamuuliza hao waliosema walipanga kufanya fujo Je mliwachukulia hatua yoyote kwasababu machafuko yalitokea? Akajibu kuwa HAPANA, hakuna hatua walichukua. Waheshimiwa Majaji, ushahidi wa wahalifu wa aina hii una uzito gani KISHERIA? Huu ndio ushahidi wa Serikali dhidi yangu. Ushahidi wa wahalifu waliokiri tutafanya uhalifu wakaja Mahakamani wakakiri. Wakarudi walikokuwa wanapanga na baadae watu wakauwawa wengi huko mitaani. Ushahidi wa aina hii una uzito gani kwenye kesi ya uhaini? Mashahidi wa aina hii ni totally unreliable. Nitaleta kwa maandishi hoja hizo za kisheria. Waheshimiwa Majaji shitaka linasema nilitengeneza nia ya kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nikathibitisha nia hiyo kwa kutamka yale maneno maarufu. Anatizama juu Mwenyekiti Lissu na kuonesha hawa watu ni wajinga sana. Ngoja tusikie ataendeleaje hapo.....kuna kaukimya kidogo. 😂 Sasa Waheshimiwa Majaji kuhusiana na shitaka hili na kwa mujibu wa maamuzi ya kisheria tuliyozungumza sana kitu cha muhimu ni uwepo wa nia ya kutenda kosa la uhaini. Ushahidi wa Jamhuri unasemaje kuhusu hiyo nia ya kutenda kosa la uhaini? Mashahidi waliotoa ushahidi kuthibitisha hoja hii ni hawa wafuatao. PW1, PW2, PW16 na PW17 ambae ni P yule mwandishi kwa ridhaa yenu naomba nipatiwe exhibit D1, D15 na D16. Kimya kidogo kinapita. Majaji wanaandika na hizo exhibit zinatafutwa. Ushahidi wa PW 1 George Bagyemu Msaidizi wa Mafwele kuhusiana na nia ya kutenda kosa la uhaini inayodaiwa katika hati ya mashitaka kwenye ushahidi wake alisema kwamba mimi nilitengeneza nia ya kuitishia serikali. Aliona nia ya kutenda kosa la uhaini katika kauli niliyotoa. Nia aliiona kwenye maneno yeye. Waheshimiwa Majaji shahidi mwingine aliyeona nia hiyo ni PW 16 Amin Mahamba. Waheshimiwa Majaji Exhibit D15 maelezo yake Polisi alisema huyu Mahamba akasema hivi "Mimi pamoja na timu nzima ya upelelezi tuliitizama na kuiskiliza video hiyo tukabaini kuna kosa la uhaini na kuchapisha taarifa za uongo." Part 280 itaendelea kwenye post inayofuata Naomba Repost yako.
3
25
96
5,951
TUJIELIMISHE ILI KUJISAHIHISHA. KESI YA LISSU: HAKUSHINDWA BALI MAHAKAMA ILIAMUA KUWA ANA KESI YA KUJIBU HIVYO UTETEZI UNAFUATA. Pamoja na kuheshimu uamuzi wa Mahakama, mimi ninaendelea kuhimiza busara na hekima zitumike katika ngazi zote za maamuzi ili taifa letu liondokane na jambo hili la kusikitisha. Tuweze kuambizana ukweli, kusameheana na kuridhiana. Sizungumzii hatia au kutokuwa na hatia kwa Lissu; hilo ni jukumu la Mahakama. Ninazungumzia mazingira ya kesi hii, historia yetu na umuhimu wa sheria kutumika kwa usawa. Tutambue: 1. Kesi ya Tundu Lissu ina tofauti kubwa na kesi nyingi za uhaini zilizowahi kutangulia hapa nchini. Katika kesi hizo za kihistoria kulidaiwa kuwepo njama, washirika, mipango ya pamoja ya kuipindua Serikali, na katika baadhi ya kesi washirika kutoka jeshini na madai ya kupanga kumuua Rais. Katika kesi hii Lissu ameshtakiwa peke yake, na kiini cha shtaka kinahusu kauli zake za hadharani. Hii ni tofauti muhimu inayostahili kutafakariwa bila kuingilia kazi ya Mahakama. 2. Lissu anashitakiwa kwa uhaini chini ya kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu, kutokana na kauli alizotoa katika mkutano wa CHADEMA tarehe 3 Aprili 2025. Kaulimbiu yake ilikuwa “No Reforms, No Election.” Upande wa mashtaka unadai kwamba kauli zake kuhusu “kukinukisha”, kuzuia au kuvuruga uchaguzi zilivuka mipaka ya siasa za kawaida. Kauli hizo ni kali. Lakini katika historia ya siasa zetu tumewahi pia kusikia kauli kali zaidi. Mfano wimbo maarufu: “Wapinzani tuwashike, tuwachanechane, tuwatupe.” Hata Bungeni wimbo huo uliwahi kulalamikiwa lakini ikachukuliwa ni utani wetu wa jadi. Pia mitandaoni leo tunasikia kauli za kutishia watu, kuwaua au kuwapoteza bila hatua zinazoonekana kuchukuliwa kwa kiwango sawa. Ndiyo maana wapo wananchi wanaojiuliza: Je, sheria inatumika kwa usawa kwa kauli za wanasiasa wa pande zote? Bibi yangu aliwahi kunikanya kuwa :Ukitania uwe tayari kutaniwa". 3. Lissu alitoa matamko yake hadharani au katika mikutano ya kisiasa. Wananchi wengi waliyasikia na wanayajua. Kwa hiyo, pamoja na kuacha Mahakama ifanye kazi yake kwa uhuru, ni vigumu kuzuia mjadala wa wananchi kuhusu jambo ambalo liko hadharani na linagusa siasa, sheria na haki za kiraia. Ili mradi staha izingatiwe na mjadala huo usibadilishwe kuwa hukumu ya hatia au kutokuwa na hatia kabla ya Mahakama kumaliza kazi yake. 4. Kama Mahakama ingelikuwa imeamua kuwa hakuna kesi ya kujibu, hatua ya utetezi isingefunguliwa. Sasa Lissu ameomba kuwaita baadhi ya viongozi wakuu, akiwemo Rais Samia na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, kutoa ushahidi. Historia ya nchi nyingine inaonyesha kuwa jambo la Rais aliye madarakani kutoa ushahidi katika shauri la jinai lina utata lakini si geni kabisa. Mwaka 1807, katika kesi ya uhaini ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Marekani Aaron Burr, Burr aliomba ushahidi kutoka kwa Rais Thomas Jefferson, bosi wake. Jaji Mkuu John Marshall ndiye alikuwa muamuzi na alikataa "dhana kwamba Rais ana kinga ya moja kwa moja dhidi ya mchakato wa Mahakama pale ushahidi wake unapohitajika katika kesi ya jinai". Jefferson hakulazimishwa kusimama mwenyewe kizimbani, lakini alitoa ushahidi kwa nyaraka na kanuni muhimu ikawa: hadhi ya Urais haimaanishi kwamba ushahidi muhimu kwa mtuhumiwa hauwezi kupatikana. Baadaye, Marais wengine wa Marekani wamelazimika kutoa ushahidi au taarifa katika mashauri ya jinai inapohitajika. Ni pamoja na: James Monroe — 1818 Ulysses S. Grant — 1876 Gerald Ford — 1975 Jimmy Carter — 1978 Jimmy Carter tena — 1980 Bill Clinton — 1996 Richard Nixon mwaka 1974 aliamriwa kutoa kanda za Watergate. Mara nyingi ushahidi huo ulitolewa kwa maandishi, nyaraka, viapo/deposition au video badala ya Rais kufika mwenyewe mahakamani. 5. Hakika Hatua inayofuata katika kesi ya Lissu ni nyeti. Itatuonyesha mwanga katika masuala haya muhimu kuhusu utawala wa sheria na haki ya mshitakiwa kupata utetezi stahiki. 6. Kiuhalisia Wengine tumejikita kwenye swala la HEKIMA, BUSARA na HURUMA YA MUNGU.
86
356
14
1,141
46,392
Pale ambapo umehudhuria tukio la pete ya uchumba ya Binti wa Rais wa Kenya, William Samoei Ruto na wakati wa kurejea Nyumbani unaendeshwa na Rais hadi kwenye usafiri wako, hicho ndicho kilichomtokea Mfanyabiashara Tajiri wa Zimbabwe, Sir Wicknell Chivayo. Katika taarifa hiyo iliyopachikwa mtandao leo Agosti 10, 2026 Chivayo amesema baada ya kuhudhuria sherehe hiyo, hakutarajia siku yake ingeendelea kuwa ya kipekee zaidi kwani wakati akiondoka Rais Ruto alijitolea kumwendesha kwa umbali wa takribani kilomita tatu hadi kwenye eneo alipoiacha helikopta yake kwa ajili ya kurejea nyumbani. Bilionea huyo amesema aliketi kwenye kiti cha mbele cha abiria huku mkewe akiwa nyuma, wakati Rais Ruto akiwa dereva, amesema kitendo hicho kimemwacha akiwa amejawa na furaha na mshangao, akitafakari jinsi alivyopata fursa ya kuendeshwa na Mkuu wa Nchi mwenyewe. Pia Chivayo, amesema kuwa amewahi kupitia matukio mengi ya kifahari na ya kipekee, lakini tukio hilo lilikuwa la kwanza kwake na limemgusa kutokana na unyenyekevu na ukarimu alioonyeshwa na Rais Ruto, huku akimshukuru Rais huyo kwa upendo na wema aliomwonyesha, akisema safari hiyo itabaki kuwa miongoni mwa safari za thamani zaidi kwake. #MillardAyoUPDATES
10
18
3
314
53,590
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewataka Wazazi na Walezi kuzingatia malezi ya Watoto kwa kuwajengea misingi ya kumpenda Mungu, kufanya kazi na kusoma. Akizungumza katika Ibada ya Misa Takatifu Maalum ya Wanajumuiya wa Uru Seminari, iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Kristo Mchungaji Mwema-Tabata Kimanga, Jijini Dar es salaam, Nchimbi amesema Jamii inapoteza eneo kubwa katika malezi ya Watoto wa siku hizi. Amesema Watoto wanapaswa kufundishwa kumpenda Mungu, kufanya kazi na kusoma, akisema baadhi yao wamejikita zaidi katika michezo ya mtandaoni badala ya masomo. “Kanuni kuu tatu, sala, kazi na masomo, tuwafanye Watoto wajue na kumpenda Mungu, tufanye Watoto wetu wapende kufanya kazi, siku hizi Watoto wengi wanapenda game hivyo tuwafanye wapende kusoma kwani kutosoma kunawafanya wapende njia za mkato,” amesema Nchimbi. Aidha, amesema Serikali itaendelea kuthamini mchango wa Taasisi za Dini katika Jamii. #MillardAyoUPDATES
3
13
1
240
34,780
fm_☄ retweeted
Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Tanzania inatambua Jeshi la Polisi tu kama chombo pekee cha kufanya UPELELEZI/UCHUNGUZI wa makosa ya jinai & Ofisi ya DPP ndiyo yenye MAMLAKA ya kuanzisha mashtaka. Hii inayoitwa tume ya uchunguzi wa jinai ya #MO29, italeta MGOGORO na nahisi itatokea hivi; tume itapokea taarifa za UKWELI toka kwa wananchi, mtawala ataikataa, halafu taarifa itafanyiwa MABADILIKO ya UONGO ili mtawala afurahi. Lakini, kisheria ni kwamba, DPP akifungua mashtaka dhidi ya mtu au kikundi cha watu, basi hao wajumbe wa tume itabidi waje KUTOA USHAHIDI mahakamani kwa sababu wanahusika kwenye ule MNYORORO wa kupatikana kwa ushahidi (chain of custody/evidence). Ikitokea wajumbe wakasema uongo, hapa ndipo tutaleta wananchi waliotoa taarifa kwa tume hiyo kufanya COUNTER-ATTACK ya kibabe. Binafsi, naomba Mungu hili suala lifike mahakamani ili ifungue PANDORA BOX ya yaliyomo kwenye ile tume ya Jaji Chande pia. Moto mzito utawaka!!
15
91
1
282
24,619
Nafikiri nitaeleweka kirahisi. Tujadili kuhusu; Commission of Inquiry into the Post-Election Violence (CIPEV), chini ya Jaji Philip Waki, Waki Commission (Tume ya Waki) iliundwa kwa tangazo la Gazette Notice ya Rais Mwai Kibaki, Terms of reference (ToR) zake zilitangazwa katika Kenya Gazette Notice No. 4473 ya 22 Mei 2008 Tume hiyo ilikuwa na jukumu la: 1. Kutafuta na kuchunguza chanzo na mazingira yote ya ghasia zilizofuata uchaguzi mkuu wa 2007. 2. Kuchunguza vifo, ukiukwaji wa haki za binadamu na uharibifu wa mali uliotokea wakati wa ghasia. 3.Kuchunguza mwenendo wa vyombo vya usalama, ikiwa ni tuhuma za matumizi ya nguvu kupita kiasi. 4.Kubaini watu waliobeba jukumu kubwa katika kupanga, kuchochea au kutekeleza vurugu. 5.Kutoa mapendekezo ya namna ya kuzuia vurugu kama hizo zisijirudie katika chaguzi zijazo tena. 6.Kupendekeza namna ya kuwawajibisha wahusika wa makosa makubwa yaliyofanyika katika vurugu. Hii tume yenu ya jana, majaji wa Uganda; ToR zake zimetangazwa gazeti la Serikali au zinatoka tu kwa mtu aliyeunda tume na kuteua wajumbe? Kwanini hii tume yenu haitaki kabisa kuweka ToR ya kuchunguza mwenendo wa vyombo vya usalama? Au, matumizi ya nguvu yalikuwa kidogo tu? Nafikiri, waliopiga watu risasi, wanatakiwa kuchunguzwa. Tume hiyo chini ya Jaji Philip WAKI iliundwa katika mazingira ya National Accord ya mwaka 2008, National Accord iliyofikiwa baada ya mgogoro wa uchaguzi kati ya Mwai Kibaki na Raila Odinga, Lakini kitu cha muhimu zaidi katika mchakato huo, usuluhishi huo ulifanyika chini ya Kofi Annan. Ripoti yake, iliyojulikana kama Waki Report, ilipendekeza mambo mengi hadi kufikia muafaka Baadaye, suala hilo lilihusishwa na kesi zilizofikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC). Ripoti ya Waki iliwasilisha majina ya wahusika wote wa vurugu na nyaraka nyingine kwa Koffi Annan, Baada ya Serikali ya Kenya kushindwa kuanzisha mfumo wa ndani wa kuwawajibisha wahusika, Koffi Annan aliwasilisha nyaraka za tume kwa Mwendesha Mashtaka wa ICC, Luis Moreno Ocampo, Mahakama ya ICC iliidhinisha rasmi uchunguzi kuhusu ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya. Kenyatta, William Ruto, Francis Muthaura, Henry Kosgey, Joshua Sang na Hussein Ali, wakashtakiwa Uhuru alikuwa upande wa PNU/Kibaki, wakati Ruto alikuwa mshirika muhimu wa ODM/Raila Odinga. Hata hivyo, ICC iliwahusisha wote wawili na wenzake katika makundi tofauti ya madai kuhusu ghasia hizo. Henry Kiprono Kosgey alikuwa Waziri wa Viwanda (Minister for Industrialization) Serikali ya Kenya. Mohammed Hussein Ali alikuwa Commissioner of Police (Mkuu wa Jeshi la Polisi Kenya) 2004 - 2009. Francis Kirimi Muthaura alikuwa Mkuu wa Utumishi wa Umma na Katibu wa Baraza la Mawaziri - Kenya. Hapa kwenu kabla hata ya usuluhishi, mnatengeneza tume na kuweka ToR za kushughulikia msiowapenda. Kwanini hamtaki kuweka ToR za kuwachunguza waliotoa amri na kutekeleza amri za mauaji ya raia? MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
16
104
500
31,465