Efficiency (@EfficiencyM) header
Efficiency (@EfficiencyM) profile picture

CEO at E-LAB RECORD'S.

Tanzania@Dar es salaam
Joined January 2013
Photo by Efficiency (@EfficiencyM)
Gerson Msigwa akiwa msemaji wa serikali ya Tanzania, alisema Nape Nnauye na wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wanashawishi Instagram kuleta na kufungua ofisi zao Tanzania. Ofisi za Instagram za kazi gani Gerson Msigwa? Tanzania tuna kazi gani na Ofisi za Instagram? Au mnataka kodi ya bluetick? Tumieni akili ndogo mlizonazo kushawishi kampuni kubwa za utengenezaji magari na vyombo vya moto kuwekeza Tanzania. Washawisji TOYOTA, Volkswagen, Mercedes-Benz, Ford, Jeep, Hyundai, Mitsubishi, Renault, Peugeot, Honda, BanBros, Subaru, Range Rover, BMW, TVS, wafanye assembling Tanzania. Mfano, gari zilizoshushwa kutoka katika meli ya mizigo 9 April 2022 katika bandari ya Dar es Salaam, gari 1,105 (sawa na 27%) ya mzigo ulioshushwa bandarini zilibaki Tanzania na gari 2,936 (73%) zilikwenda nchi jirani (Sudan, Zimbabwe, Mozambique, Malawi, Zambia). Mkurugenzi wa mamlaka ya bandari Tanzania anasema, kuanzia April 5 hadi April 7 (ndani ya siku 3 tu) bandari ya Dar es Salaam ilipokea meli nne zenye jumla ya magari 8,384 (ukilinganisha na mwaka 2021, walikuwa wakipokea gari 10,000 kwa mwezi mmoja). Hilo siyo jambo la kujivunia. Tumeamua kuifanya nchi yetu soko la magari ta mtumba (used cars) kwa sababu ya kupenda tozo na kodi. Gari ambayo utaagiza kwa $4,175 (Sh9.82 milioni) utalipa kodi TRA sawa na gharama za uagizaji gari hilo. Kwamba kodi ni sawa na gharama za kununua. Serikali ya Tanzania katika gari ambalo mtanzania ananunua, haiweki hata ‘spare tyre’ lakini wanachukua kodi sawa na bei uliyonunua gari yako. Huo ni WIZI na UJAMBAZI. Ndiyo maana nafikiri ni wakati sahihi sasa kampuni za magari kuwekeza viwanda vya kuzalisha magari yao Tanzania. Kenya imetengeneza sera - National Automotive Policy (NAP) iliyoanzishwa mwaka 2019 ili kuimarisha sekta ya utengenezaji magari ndani ya Kenya, ikitaka kuongeza uzalishaji maradufu kufika mwaka 2025. na kupunguza utegemezi wa magari mitumba (used cars) kutoka nje ya Kenya. Sera hiyo inatoa mazingira wezeshi kwa wadau wa sekta ya kuuza na kutengeneza magari kufikia uwezo wao kamili na nafasi ya Kenya kama mtengenezaji mkuu wa magari, ukanda wa Afrika Mashariki, eneo ambalo ni soko kubwa (jalala) la magari mtumba (used cars) kutoka Europe na Japan. Sera inatatua ukosefu wa mifumo maalum ya kisheria, mfumo wa kitaasisi na udhibiti, wamiliki wageni waliothibitishwa kuagiza vifaa na bidhaa, na kudhibiti utitiri wa magari yaliyotumika (used cars). Pia, kufanya tasnia ya kutengeneza a kuuza magari ya ndani kuwa na ushindani. Sekta hii ya kutengeneza na kuuza magari imeweza kutoa ajira zaidi ya 100,000 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kwa wananchi wa Kenya. Sekta hiyo pia inachangia takribani Ksh30 bilioni (Sh518.38 bilioni) kwa mwaka kwa serikali kupitia ushuru na kodi. Wakati majirani Kenya wanafikiria hivi, serikali ya CCM inamuagiza msemaji wa serikali aende kwenye kipindi cha Radio, awaeleze watanzania kwamba serikali kupitia wizara na waziri wa habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wanawashawishi INSTAGRAM kuweka ofisi zao Tanzania. Ulimwenguni, tasnia hii ya kutengeneza na kuuza magari imekuwa nguzo ya ukuaji wa uchumi wa viwanda na kichocheo kikuu cha ukuaji wa uchumi mkubwa na maendeleo ya kiteknolojia. Serikali ya Tanzania inatakiwa kuwekeza akili huku siyo kuwa kichekesho cha Ulimwengu. Associated Vehicle Assemblers (AVA) ndiyo kampuni kubwa zaidi ya kutengeneza magari nchini Kenya, inayofanya kazi kwa chapa kama vile MITSUBISHI Motors, SCANIA, TATA, HINO na TOYOTA. Kampuni hiyo hapo awali ilikuwa ikitengeneza pia magari ya PEUGEOT, FIAT, IVECO na VOLVO (malori) Associated Vehicle Assemblers (AVA) Ilichukuliwa na Simba Corporation mwaka 2017 kwa ubia na Marshalls East Africa na kukarabatiwa kwa Ksh4 bilioni (Sh69.15 bilioni). 2022 walitengeneza magari 7,500. AVA inatengeneza magari ya TOYOTA na MAHINDRA katika kiwanda cha Mombasa. Mwaka 2021 wametangeneza magari 300 kwa ajili ya Jeshi la Polisi Kenya kwa gharama ya wastani ya Ksh2.5 milioni (43.25 milioni) na kutengeneza daladala (matatu) 3,600 zenye viti 16 (kila moja). 2022 wakatengeneza magari 132 ya MAHINDRA kwa Polisi. Magari yote yanaundwa Kenya. Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Kenya (KNBS) inasema katika ripoti yake kwamba idadi ya magari yaliyotengenezwa nchini Kenya iliongezeka kutoka magari 3,241 mwaka wa 2018, hadi kufikia magari 4,406 mwaka wa 2019, kati ya miezi ya Januari na Julai. TOYOTA (Japan) wanatengeneza LandCruiser na Hilux, RENAULT (France) wanatengeneza malori. Serikali ya Kenya imetoa agizo Taasisi na Idara za serikali kununua magari kutoka ndani kwa ajili ya shughuli mbalimbali. Hii inapunguza uagizaji wa magari ta serikali kutoka nje ya Kenya. Hii sio tu nzuri kwa kuongeza uwezo wa utengenezaji wa magari (kwa watu wa Kenya) lakini pia ni nzuri katika suala la uhamisho wa ujuzi (skills transfer), katika suala la kuunda ajira kwa watu wao na katika kuunda fursa mpya (creating new opportunities). Kwa namna gani? Kuna watu wanatengeneza brakepads, windscreen, suspensions & shock absorbers. Wote watapata ajira rasmi katika viwanda au kuuza ujuzi wao, kuna watu watauza mipira kwa ajili ya magurudumu, wakulima wataanza kulima zao la mpira (Hevea brasiliensis). Faida itakwenda mbali zaidi. Kutengeneza bidhaa kama matairi, viatu na gloves. Mahitaji ya soko ni 99.7% ambalo kwa sasa mauzo ya zao hilo ni 0.03% pekee. Kama tunaweza kuwashawishi wenye viwanda vya magari kuwekeza Tanzania, wakulima wetu hawajanufaika? RENAULT wanaunda K-Range heavy-duty trucks, Renault walitumia Ksh58 milioni (Sh1 bilioni) kufanya maboresho ya uzalishaji wao eneo la Thika. Hii ni sawa na pesa ambayo makamu wa Rais wa Tanzania ametumia kukarabati ofisi zake Dodoma na Dar es Salaam. MMM, Martin Maranja Masese
148
237
18
1,556
184,333
Mpigie kura Cindy Rulz ashinde tuzo za UMA’s, ‘Best International Artist’ - Bongo5.com bongo5.com/cindy-rulz-atajwa…
Some crazy beat battles inside U.S youtu.be/GmWaASn2Ufo via @YouTube
Replying to @BBCAfrica
These people who transported them are Fools, the pic shows exactly how their brain thinking capacity is retired.@BBCAfrica
‘Love takes time to heal'.@(Prod by Tonny/Efficiency Man)’ by @EfficiencyM on #SoundCloud? soundcloud.com/efficiency-ma…
Wiz Khalifa - "The Plan" ft. Juicy J (Official Video): youtu.be/x8Oha-TnekE via @YouTube
God bless the work of my hands, Amen.
The night may be too long but the day will come#self thoughts.
having a nice sea view, nice wind blowing, its really a great weekend.
Pregnancy Test Frog May Have Spread Fatal Fungus - Yahoo! News news.yahoo.com/pregnancy-tes… via @YahooNews
Brain is the greatest asset ever existed, i thank the might creator for that creation.
Success is all about your attitude and efforts over something never expect miracles.