EVENING WORD
SERMON: INTERPRETATION OF DREAMS
The gift of interpreting dreams enriches a person's salvation and helps build the love of God within them. When you have this gift, you will love God, and whenever He speaks, you will be able to hear His voice because of your love for Him. When you understand how to interpret dreams, it becomes much easier for you to experience the goodness of God.
The goodness of God is constantly at work, but many people fail to experience it because they do not understand how to interpret it. If you fail to understand the meaning of your dream, you may miss the opportunity to respond appropriately. To understand God's messages and the dreams you receive, you need to have the Spirit of God within you to guide and help you.
©️ Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira
34
NENO LA JIONI
SOMO: TAFSIRI YA NDOTO
Kipawa kwa ajili ya waota ndoto hupendezesha wokovu wao na kujenga upendo wa Mungu ndani yao. Ukiwanacho utampenda Mungu na wakati wote utakapokuwa akisema utamsikia kwa sababu unampenda. Ukijua kutafsiri ndoto ni rahisi sana kwako kupata wema wa Mungu.
Mara zote wema wa Mungu hutembea lakini watu hawaupati kwa sababu hawaelewi tafsiri yake. Usipoelewa tafsiri ya ndoto yako utashindwa kuitikia. Ili uweze kuelewa ujumbe wa Mungu na ndoto unazoota ni lazima uwe na Roho wa Mungu ndani akusaidie.
©️ Mtume na Nabii josephat Elias Mwingira
NENO LA SIKU
Na, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira – Kanisa la Efatha
TAREHE: 18/11/2026
SOMO: USIKUBALI KUSHINDWA
Maisha ya wokovu ni maisha ya uaskari, sio maisha ya lelemama au ulegelege. Ni maisha ya mtu aliadhamiria kwenda mbele. Unapokabiliwa na dhambi, aibu au kushindwa, usiseme, “Mimi siwezi.” Sema, “Bwana, nitie nguvu niweze kushinda.”
Katika kutafuta ushindi wako, usijitiishe chini ya ufalme wa giza wala kukubali kutawaliwa na dunia. Amka, simama imara, upige vita vizuri vya imani, kama Neno linavyotuagiza katika 1 Timotheo 6:12.
Hata jambo linapoonekana kuwa gumu kulishinda, usiseme, “Nimeshindwa.” Mwambie Bwana, “Nitie nguvu, unipe ushindi.” Kumbuka neno hili la Wafilipi 4:13, “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.”
Ita usaidizi, lakini usisalimu amri, hatakama changamoto hiyo inakuzidi umri, yupo aliye na umri mkubwa kuliko hilo tatizo.
WORD OF THE DAY
With, Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira – Efatha Church
DATE: 18 November 2026
SERMON: REFUSE TO ACCEPT DEFEAT
The life of salvation is the life of a soldier. It calls for discipline and a determination to press forward. When you face sin, shame, or failure, do not say, “I can’t.” Say, “Lord, give me the strength to overcome.”
As you seek victory, refuse to submit to the kingdom of darkness or let the world rule over you. Rise up, stand firm, and fight the good fight of faith, as the Word instructs us in 1 Timothy 6:12.
Even when something seems hard to overcome, do not say, “I’ve been defeated.” Tell the Lord, “Strengthen me and give me victory.” Remember these words from Philippians 4:13, “I can do all things through Him who strengthens me.”
Call for help, but do not surrender. Even if that challenge is older than you, there is One who is older than the challenge itself.
UKIRI WA SIKU.
NAIBARIKI JUMATANO YANGU.
Mimi nitakopesha maana nitakuwa na UTELE. Mimi Nimebarikiwa na BWANA.
Asante YESU, Asante BABA, Asante ROHO MTAKATIFU.
DECLARATION OF THE DAY.
I BLESS MY WEDNESDAY.
I shall lend, for I will walk in ABUNDANCE. I am Blessed by the LORD.
Thank You, JESUS. Thank You, Lovely Heavenly FATHER. Thank You, HOLY SPIRIT.
3
66
NENO LA SIKU
Na, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira – Kanisa la Efatha
TAREHE: 17/11/2026
SOMO: MJUE MUNGU KWANZA
Ayubu 22:21 “Mjue sana Mungu, ili uwe na amani. Ndivyo mema yatakavyokujia.”
Mahitaji yako yatatimizwa na Mungu baada ya kumjua Yeye. Watu wengi hujishughulisha kutafuta fedha ili wawe vile wanavyotamani kuwa, lakini hawatengi muda wa kutosha kumtafuta Mungu.
Kadiri unavyomfahamu Mungu, ndivyo unavyopokea kile ambacho ni stahiki yako. Kwa jinsi unavyomfahamu, kwa kiwango hicho hicho utapokea kile ambacho ni stahiki yako.
Siku utakapoelewa kwamba Mungu ndiye aliyekuumba na kukuweka katika bustani aliyoipanda ili uitunze, ndipo utakapofahamu kwamba wewe ni tajiri. Akili yako ikiendelea kukuambia kwamba wewe ni maskini, fikra hizo zitakuzuia kufikia hatua ambayo Mungu alikuumbia uifikie.
Chochote unachomiliki, unakimiliki kwa niaba ya Muumbaji. Yeye ndiye aliyeviumba vyote, nawe amekukabidhi jukumu la kuvitunza.
WORD OF THE DAY
With, Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira – Efatha Church
DATE: 17/11/2026
SERMON: GET TO KNOW GOD FIRST
Job 22:21 “Get to know God well, so that you may have peace. Then good things will come to you.”
As you come to know God, He will meet your needs. Many people keep themselves busy pursuing money so they can become who they want to be, but they set aside too little time to seek God.
The more you know God, the more you receive what is rightfully yours. What you receive is in proportion to how well you know Him.
The day you understand that God created you and placed you in the garden He planted so you could tend it, you will realize that you are rich. If your mind keeps telling you that you are poor, those thoughts will keep you from reaching the place God created you to reach.
Whatever you own, you hold on behalf of the Creator. He created it all and entrusted you with the responsibility of caring for it
UKIRI WA SIKU.
NAIBARIKI JUMANNE YANGU.
Upendo wa BWANA umetuzunguka, Familia yangu ni Salama, hakutakuwa na magomvi wala magonjwa wala vifo, wala ukata. Mimi na Familia yangu TUMEBARIKIWA na BWANA.
Asante YESU, Asante BABA, Asante ROHO MTAKATIFU.
UKIRI WA SIKU.
NAIBARIKI JUMATATU YANGU.
Mimi ni Mshindi siwezi kushindwa. Mjini sitashindwa, Vijijini sitashindwa. Mimi NIMEBARIKIWA.
Asante YESU, Asante BABA, Asante ROHO MTAKATIFU.
Kuna mengi yamechukua muda wako wiki hii; Jumapili hii, tenga muda wa kuwa nyumbani mwa Bwana.
Tunakukaribisha kesho, tarehe 15 Novemba 2026, saa 2:00 asubuhi, Efatha Church Mwenge, Dar es Salaam.
Mpe Mungu nafasi ya Kwanza, Usichelewe Ibadani.
#EfathaChurch
#SundayService
NENO LA SIKU
Na, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira — Kanisa la Efatha
TAREHE: 14/11/2026
SOMO: KUWAHI IBADANI.
Zaburi 122:1 “Nalifurahi waliponiambia, Na twende nyumbani kwa Bwana.”
Furaha ya kuwahi ibadani huleta neema ya kipekee kutoka kwa Mungu. Wanaompenda Mungu huona fahari kuwa katika nyumba yake mapema. Watu wa dunia hutegemea magari na farasi, lakini wana wa Mungu hulitumainia jina la Bwana.
Bwana Yesu alisema kulikuwa na wanawali kumi ambapo watano walikuwa na hekima na watano walikuwa wapumbavu. Wenye hekima walikuwa na mafuta yao lakini wapumbavu walikuwa hawana mafuta. Alipofika Bwana harusi wao ikabidi wakimbie kutafuta mafuta na waliporudi wakakuta wamechelewa na mlango umefungwa.
Unaweza kuwa mwaminifu katika kazi yako, biashara au masomo, lakini inapokuja katika mambo ya Mungu unachelewa. Mwana wa Mungu, usichelewe Kanisani, maana katika mkutano wa watakatifu, Mungu ndiye mwenyeji na mkuu wa mkutano. Kuchelewa ni ishara ya kutomheshimu Mungu na kusababisha wewe uchelewe kupokea. Inaweza kuonekana ni jambo dogo, lakini kuna Baraka ya kipekee kwa wanaowahi kwa sababu Mungu anaona heshima yako, naye atakuheshimu pia.
WORD OF THE DAY
With, Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira — Efatha Church
DATE: 14/11/2026
SERMON: ARRIVING EARLY FOR WORSHIP.
Psalms 122:1 “I was glad when they said unto me, Let us go into the house of the Lord.”
The joy of arriving early for worship brings special grace from God. Those who love God take pride in being in His house early. The people of the world trust in chariots and horses, but the children of God trust in the name of the Lord.
The Lord Jesus spoke of ten virgins: five were wise and five were foolish. The wise had oil, but the foolish had none. When the bridegroom arrived, the foolish virgins had to rush out to find oil. When they returned, they found that they were too late and the door had been shut.
You may be faithful in your work, business, or studies, yet when it comes to the things of God, you arrive late. Child of God, do not be late for church, for in the gathering of the saints, God is the host and presides over the assembly. Arriving late is a sign of disrespect for God and delays your receiving from Him. It may seem like a small matter, but there is a special blessing for those who arrive early, because God sees the honour you give Him, and He will honour you too.
UKIRI WA SIKU.
NAIBARIKI JUMAMOSI YANGU.
Mimi niko SALAMA; Hakuna cha kunidhuru. Jumamosi yangu Imebarikiwa na BWANA.
Asante YESU, Asante BABA, Asante ROHO MTAKATIFU.
EVENING WORD
SERMON: HOPE BRINGS LIFE AND A FUTURE
When you put your trust in God, you will be established, because hope brings life, the ability to live and a future. This is why God says: Jeremiah 29:11 “For I know the thoughts that I think toward you, saith the LORD, thoughts of peace, and not of evil, to give you an expected end.” Knowing this, the devil has become very cunning and deliberate in deceiving people, with the intention of destroying them and leading them away from their true identity and purpose.
When a person remains true to who God created them to be, they will fulfil God's will. This is what makes them a great and glorious person for the sake of God's Kingdom. However, when the devil succeeds in trapping someone, he leads them astray and prevents them from fulfilling God's will any longer.
©️ Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira
NENO LA JIONI
SOMO: TUMAINI HULETA KUISHI NA UBAADAYE
Unapomtumaini Mungu utathibitika kwa sababu tumaini huleta uhai, kuishi na ubaadaye; ndiyo maana Mungu anasema; Yeremia 29:11 “Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.”
Shetani kwa kujua hili amekuwa makini na mwerevu kumdanganya mtu ili aharabikiwe aondoke katika uhalisi wake. Anapokuwa katika uhalisia wake atatimiza mapenzi ya Mungu ndipo anakuwa mtu mkuu na mwenye utukufu kwa ajili ya ufalme wa Mungu. Shetani akifanikiwa kumnasa, humwendesha asiweze kutimiza mapenzi ya Mungu tena.
©️ Mtume na Nabii josephat Elias Mwingira
NENO LA SIKU
Na, Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira – Kanisa la Efatha
TAREHE: 13/11/2026
SOMO: UNAONA NINI MBELE YA TATIZO LAKO?
Wapelelezi kumi na wawili walienda kuipeleleza nchi. Waliporudi, wale kumi walisema, “Majitu yale yatatuangamiza.” Wale wawili wakasema, “Hao ni chakula chetu.” Mungu alikuwa akiwasikiliza. (Hesabu 13 na Hesabu 14)
Wote waliona majitu yale yale. Wale kumi waliona ukubwa wa majitu, huku wale wawili wakiona ukuu wa Mungu aliyeyaumba. Mungu anasema, “Kwa kadiri ulivyoona, ndivyo itakavyokuwa.”
Je, unaelewa kuwa Mungu ni mkuu kuliko tatizo lako? Kama unaelewa, hongera. Kama bado hujaelewa, hongera pia.
Mungu anasema, “Kile unachokielewa ndicho fungu lako.”
WORD OF THE DAY
With, Apostle and Prophet Josephat Elias Mwingira – Efatha Church
DATE: 13/11/2026
SERMON: WHAT DO YOU SEE WHEN YOU FACE YOUR PROBLEM?
Twelve spies went to scout out the land. When they returned, ten of them said, “Those giants will destroy us.” The other two said, “They are bread for us.” God was listening to them. (Numbers 13 and Numbers 14)
They all saw the same giants. Ten saw how big the giants were, while two saw the greatness of the God who created them. God says, “As you have seen it, so it shall be.”
Do you understand that God is greater than your problem? If you do, congratulations. If you don’t understand it yet, congratulations to you too.
God says, “What you understand is your portion.”































