Pinned Tweet
ONGEZEKO LA SAFARI ZA SGR KUANZIA SEPTEMBA 01, 2026!
Tumeongeza idadi ya safari kati ya Dar es Salaam na Dodoma ili kukupa urahisi zaidi wa kupanga Safari zako kila siku.
Sasa una fursa ya kuchagua muda unaokufaa, kagua ratiba kuona muda wa kuondoka na kuwasili wa treni zetu.
Zoezi la utwaaji wa ardhi kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) linaendelea vyema katika Kijiji cha Nyamoli, Mkoani Kigoma, huku wananchi wakionyesha ushirikiano mkubwa.
Sweden, through @sidasweden, with technical support from Sweco, is supporting Tanzania to shape a more connected and sustainable future for Dodoma. As part of the Dodoma SGR Project Preparation Facility and Special Purpose Vehicle Pilot,
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Dkt. Charles Msonde, ametembelea Banda la TRC katika Maonesho ya Nanenane 2026 na kupongeza Shirika kwa kuendelea kutoa huduma bora za usafiri wa reli, hususani reli ya kisasa ya SGR ambayo imeendelea kuboresha ufanisi wa usafiri nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Dkt. Ladislaus Chang'a, ametembelea banda la Shirika la Reli Tanzania katika Maonesho ya Nanenane 2026 na kupata maelezo kuhusu huduma za usafiri wa abiria na usafirishaji wa mizigo kupitia reli ya kisasa na reli ya MGR.
Meneja Utafiti na Masoko wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bi. Irene Shayo, akiwasilisha mada wakati wa Jukwaa la Kuunganisha Uchumi wa Buluu, Biashara, Utalii na Fursa za Uwekezaji kupitia Reli Julai 30, 2026 visiwani Zanzibar.
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha sita kutoka Tabora hadi Kigoma.














































