Adamoo retweeted
6.11.2026: Hukumu ya TUNDU LISSU NA KUMBUKUMBU YA KESI YA MWALIMU NYERERE YA MWAKA 1958. HISTORIA INATUFUNDISHA NINI?
Leo, tarehe 6 Novemba 2026, Tundu Lissu ameshinda kesi ya uhaini lakini mahakama ikasema amepatikana na hatia ya uchochezi (incitement) na kuhukumiwa kifungo cha miaka 4. Tunamshukuru Mungu kwa kesi ya uhaini kutupiliwa mbali na kumpongeza Lissu kwa umahiri na ujasiri wake hadi kujitetea. Lakini hukumu ya uchochezi inasikitisha, inafikirisha na inatukumbusha historia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, ambaye naye mwaka 1958 alikutwa na hatia ya jinai ya kashfa (criminal libel) wakati wa harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Makosa haya mawili ni tofauti kisheria, lakini kesi hizi zinafanana katika jambo muhimu: zote zilihusu kiongozi mkuu wa upinzani aliyeshtakiwa na Serikali kutokana na kauli zake za kisiasa.
Turejee historia.
Tarehe 27 Mei 1958, Mwalimu Nyerere alichapisha makala katika gazeti la Sauti ya TANU, Toleo Na. 29, akiwakosoa Wakuu wawili wa Wilaya wa Serikali ya kikoloni kwa madai ya kutumia madaraka yao vibaya na kuihujumu TANU.
Akafunguliwa kesi ya jinai Na. 2207/1958 chini ya kifungu cha 187 cha Kanuni ya Adhabu (Penal Code). Serikali ya Uingereza ilitoa maelezo kuhusu mashtaka hayo katika Bunge lake (House of Commons) tarehe 26 Juni 1958.
Nyaraka za UN zinathibitisha kwamba Mwalimu alikutwa na hatia katika mashtaka mawili na kuhukumiwa kulipa faini ya shilingi 3,000 za Afrika Mashariki, sawa na pauni 150 za wakati huo, au kifungo cha miezi sita. Alilipa faini tarehe 12 Agosti 1958 na hakukata rufaa.
Kesi hiyo ilizua mjadala mkubwa. Wanaharakati wa kupigania uhuru huko London walihoji iwapo Mwalimu angepata haki katika mahakama za kikoloni na kudai kuwepo kwa waangalizi huru. Serikali ilikataa, ikisisitiza kuwa uamuzi wa kufungua mashtaka ulikuwa chini ya mamlaka ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Miaka 68 baadaye, tunajikuta tena tukitafakari maswali kuhusu uhuru wa kisiasa, matumizi ya sheria za jinai na nafasi ya mahakama katika mfumo wa kidemokrasia.
Pamoja na hukumu ya mwaka 1958, Mwalimu Nyerere aliendelea na harakati zake hadi Tanganyika ilipopata uhuru mwaka 1961.
Funzo muhimu ni kwamba hukumu ya jinai dhidi ya kiongozi wa kisiasa si lazima iwe mwisho wa safari yake ya kisiasa. Historia inaonesha umuhimu wa kuendeleza majadiliano (dialogue) badala ya mapambano na vurugu (confrontation).
Kwa wanaothamini demokrasia, mfumo wa vyama vingi, haki za binadamu, uhuru wa kujieleza na utawala wa sheria, hukumu ya uchochezi dhidi ya kiongozi mkuu wa upinzani inaibua maswali mazito yanayohitaji mjadala mpana wa kitaifa.
Je, mipaka kati ya ukosoaji halali wa Serikali na uchochezi wa jinai ikoje?
Je, mwanasiasa awe mpinzani au wa chama tawala atakosoa je Serikali au kudai maboresho au mageuzi bila kuhofia kutafsiriwa kuwa mchochezi?
Je, wananchi watawezaje kudai haki zao kwa nguvu ya hoja bila kuonekana wanachochea uvunjifu wa amani?
Walimu na wanataaluma tutawezaje kufundisha, kuchambua sera, kutoa mapendekezo na kukosoa mifumo ya utawala bila kuhofu kuitwa wachochezi?
Viongozi wetu wa dini watawezaje kutekeleza wajibu wao wa kinabii wa kukemea maovu na kusimamia haki bila kuonekana wanachochea waumini wao?
Uhuru wa kujieleza una mipaka yake na hauhalalishi haki ya kukashfu, kuchochea vurugu au uhalifu. Lakini ni muhimu sana kuweka mipaka iliyo wazi kati ya uchochezi wa jinai na ukosoaji halali wa kisiasa.
Iwapo sheria za jinai zitatumika kudhibiti ukosoaji halali wa kisiasa au kitaalamu, tunaweza kujikuta tunadhoofisha demokrasia, haki za binadamu, kuongeza hofu na kuzidisha mkwamo wa kisiasa na kiuchumi badala ya kuutatua.
Hukumu ya leo inatupa sababu nyingine ya kujadili kwa kina uhuru wa kujieleza, uhuru wa mahakama, haki za raia na za vyama vya upinzani na mipaka ya matumizi ya sheria za jinai katika siasa.
Ninarejea msisitizo wangu wa muda mrefu kuhusu falsafa ya Rais Samia ya 4Rs. Tujenge utamaduni wa kusikilizana na kukosoana kwa hoja
TUJISAHIHISHE
Hili suala la Tundu Lissu lingetokea Kenya kipindi ya BABA yuko hai mambo ingechemka yaani kingeumana vibaya sana,,,
Kwanza hiyo kukaa Kashoo siku 577 Wajaluo wasingekubali… Tanzania tunalinda “Amani”
Kweli Sheria ni pana sana nilikua sijui…
Kwamba unaenda Mahakamani kujitetea kwa kesi uliyoshtakiwa halafu ukahukumiwa kwa Kesi nyingine ambayo hukusomewa hapo awali…
Haya maneno lazima uwe umetahiriwa bila Ganzi na uwe na BALLS ndio unaweza kutamka
- “Toeni hukumu ambayo mmeagizwa”
- “Siombi Msamaha sina Kosa”
Yule tapeli ambaye ni Basha ake Yeriko alivyokua Kashoo kila akikumbuka Bapa, Mboriko, Mtori na Nyama Choma mwenyewe akatubu 😂😂😂
Adamoo retweeted
Majaji, kwa uamuzi huu mmejivua heshima, mmeondoa kabisa imani ya wananchi kwa mahakama na kuifedhehesha nchi yetu! Dhamiri zenu ziko wapi? Kiapo chenu kina thamani gani? Namshukuru Mungu sina undugu na yeyote kati yenu. Kila mmoja wenu abebe aibu na uwajibikaji wa uamuzi wake. Vyeo vitapita, majoho yatavuliwa, lakini fedheha ya uamuzi huu itawafuata katika historia!
Kumfanyia DHULMA Binadamu mwenzako ni DHAMBI kubwa sana mbele ya MUNGU
Hii Dunia sote tunapita na tutaiacha vile vile 💔
Kama kweli wanapambana na matumizi mabaya ya fedha za Umma hili suala la Uwanja tutegemee watu kuchukuliwa hatua zaidi ya hapo tutaona ni Business as usual….
“Mtu umekaa zako huna hili wala lile unashangaa wanakuAdd kwenye WhatsAap Group la Wazee na Maendeleo…”
Ifike muda CAG bora hata asitutangazie huo upotevu wa fedha za Umma kama hakuna utekelezaji wowote zaidi ya kuishia kwenye Hansadi za Vikao vya Bunge
Maana kila mwaka CAG anasema kuna upotevu wa Mabilioni ya fedha. Wezi na Mafisadi wanazidi kuitwa WAHESHIMIWA badala wakae JELA..
Naona Wakali wa kutetea Gharama za Ujenzi wa Viwanja vya Mpira wapo kwenye media hapo Crown fm KUTETEA kuwa ni sahihi ongezeko la gharama…
Hii Nchi hakuna Accountability watu ni WEZI
Mudi Mabriani Handas yake lazima anatafunia na GOZO sio PK,,, Mkali anagawa Wastani kwa idadi kwa kila atakaye yakanyaga 😂😂😂
Mudi Mabiiriani ameshaHandas nini naona anaruka na Janja Bonny na hataki kuelekezwa 😂
Biashara zinataka sana moyo na kuwa na Subra




