Necto Kitiga retweeted
Dah 💔
Rest in Peace Mzee Alute 🙏🏽
Loosing a sibling 😭 while detained illegally on trumped up charges! Very painful!
Poleni SANA wafiwa!
Inauma sana! Pumzika kwa amani Mzee wetu msemakweli! Huyu mtu wa kati asije akawa kahusika maana …
Na tusisikie kimama chenu kinakuja na kusema eti kwa huruma ya kufiwa anamsamehe Tundu alafu mnatarajia tumpigie makofi - alitakiwa awe ameshawaambia vikaragosi vyake wamwachie Lissu zamani angepata muda mzuri kuwa na kaka yake!
Mi ninavyo waona ninyi na roho zenu nyeusi mnaweza kuwa mme engineer kitu kama hiki kama mliweza kununua silaha nzito kuja kuua maelfu ya watanganyika hamshindwi uovu wowote!
Utawala katili na wa kishenzi huwezi kujivua ukatili wako we mtumishi wa Shetani 🚮
Poleni tena wafiwa - mzee apate kupumzika sasa 🙏🏽
Necto Kitiga retweeted
CHADEMA: Hatutashiriki katika maridhiano ya kudanganyana
bbc.in/4iMV00v
Necto Kitiga retweeted
Kuna msamaria mwema alijitokeza kumsaidia na akataka jina lake lisitajwe ni nani anafanya wema wa namna ile alafu akataka asijulikane?,
lakini akatuma waandishi wa habari wakajionyeshe kuwa wamempa msaada!
Kama hakutaka kujulikana kwanini alituma waandishi?
Pole Angel! 🕊️
Necto Kitiga retweeted
mimi nawatia moyo chadema, na kuwasihi kuendelea. nawashukuru sana, sana, kwa uwepo wao, na kwa gharama wanazoendelea kulipia, na kutulazimisha, kama taifa, kutafakari endapo kama tulianzisha vyama vingi kama mbwembwe tu au kufanikisha demokrasia ya kweli:
Necto Kitiga retweeted
Huyu jamaa amenitoa MACHOZI.
Katumia lugha nyepesi sana kuelewesha watu. Usipomuelewa huyu jamaa basi.
REPOST 200
Necto Kitiga retweeted
#MahakamaKuuMbeya
Tumefungua kesi kwa Udharura #HabeusCorpusAppln kutaka #GwamakaMbugi anayeshikiliwa na Polisi zaidi ya siku9 aletwe Mahakamani
#Badlucky Kesi imepangwa J.tatu next week
Kesi aina hii, Hupewaga kipaumbele cha kusikilizwa hata siku hiyohoyo
#UtawalaWaSheria⚖️
Necto Kitiga retweeted
Uwezo wa KIKEKE kuhoji UMESHUKA sana aisee..!
Kikeke wa BBC hapa ningetegemea maswali kadhaa kama haya;
1. Uchunguzi wa KUSHAMBULIWA kwa faza Kitima umefikia wapi?
2. Mdude , soka, Mlay, tunaenda mwaka wa pili kupo kimya.
3. Polepole aliekuwa BALOZI mpaka leo hakuna majibu ya kutekwa kwake kwanini?
Haya ni baadhi ya maswali ambayo yanatakiwa kuulizwa angle ya UTEKAJI, leo mjadala unaisha juu juu tuu kama wapo VILABUNI.
Necto Kitiga retweeted
Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Kigoma Kamanda Colletha Ntidyicha aliyeshitakiwa kwa tuhuma za UGAIDI akirudishwa Gereza la Segerea mara baada ya shitaka lake kutajwa ndani ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo.
Necto Kitiga retweeted
UJUMBE WA MUHIMU SANA HUU KWA WANACHADEMA KIPINDI HIKI.
ASANTE MAKAMU @HecheJohn
REPOST 200
Necto Kitiga retweeted
Mwaka jana kutekwa kwa kakaangu MDUDE nilipitia stress kama miezi mitatu.
Huu mwaka kwa ndugu yangu TWAHA kunanitesa sana, sijui hii haki itaisha lini.
Kwamba wapigania HAKI WOTE huu ndio mwisho wetu daah..!
LEO MOYO WANGU UNAUMA SANA.
Necto Kitiga retweeted
TAARIFA KWA UMMA
Mwenyekiti wa Jimbo la Kyela Mhe. Victoria Swebe anashikiliwa na Jeshi la Polisi tangu jana Jumatatu alipoenda kuitikia Wito wa RCO wa Mkoa wa Mbeya.
Kwa Sasa yupo Kituo cha Polisi Central Mbeya Mjini.
Necto Kitiga retweeted
Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Mwanza, Abbas Mayala amesema vijana wa chama hicho hawatashiriki mazungumzo yoyote ya maridhiano kati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) endapo Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu hatashirikishwa kuyaongoza.
Necto Kitiga retweeted
Yaani kila ninapotafakari kuhusu makosa ambayo yapaswa adhabu yake yawe kifo sipati majibu.Hivi kuwa mkosoaji wa serikali anaekubalika na jamii ni kosa ? Inawezekana waliotuingiza kwenye mfumo wa vyama vingi hawakuwaza vizuri?
Walipaswa kuwaza kuwa ipo siku atakuja mtawala ambae hatavumulia ukosoaji,walipaswa kuwaza kuwa huyu mtawala ataondoa vijana wa Tanzania kwa kuwateka na kuwapoteza kwa sababu hataki kukosolewa.
Hii haiwezi kuwa njia sahihi ya kuunyamazisha upinzani.Upinzani unanyamazishwa kwa kuwatendea haki wananchi.Upinzani utanyamaza siku Demokrasia itakapoheshimika kama mfumo bora wa kiuchaguzi.Upinzani utanyamaza Watanzania watakapopata maendeleo kwenye level za Kata bila ya mtu kuuwawa.
Upinzani hauwezi kunyamaza kama 98% ya Bunge ni la chama kimoja lakini bado hakuna maendeleo mtaani.Tunanyamaza vipi ikiwa umasikini unaongezeka uraiani lakini CAG anatoa ripoti za ufisadi wa hawa wanaojiita viongozi wa nchi?
Ajira hakuna,Maendeleo hakuna,Huduma za afya ni hafifu,Barabara ni za hovyo,Pesa hakuna mtaani na Mafuta bado yanaendela kupanda bei.Ukihoji wanakutafuta upotezwe.
IT CANT BE,WE CANT CONTINUE LIKE THIS.
Bring back Twaha Mwaipaya. Free him now.
Necto Kitiga retweeted
DAMU ZA WATU Vs DHAMIRI
Rev Peter Simon Msigwa
Nina swali kwa kila mtu aliyepewa dhamana ya kulinda haki na maisha ya watu: Jaji, Polisi, mwanasheria, kiongozi wa Serikali au mtu yeyote mwenye mamlaka.
Unajisikiaje unapojenga nyumba nzuri, unanunua gari la kifahari, unasomesha watoto wako shule za gharama kubwa, unakula vizuri na kuishi maisha ya anasa, huku ukijua kwamba huenda ustawi huo umejengwa juu ya machozi, mateso na damu za watu ambao ulipaswa kuwalinda?
Unapolala kwenye godoro la gharama kubwa, dhamiri yako inalala pia?
Unapofungua mlango wa nyumba yako nzuri, unakumbuka familia ambazo zimebaki bila baba, mama au watoto kwa sababu ya matumizi mabaya ya mamlaka?
Unapompeleka mtoto wako shule nzuri, unawafikiria watoto ambao maisha yao yamevurugika kwa sababu ya mzazi wao kunyimwa haki?
Unapoketi na familia yako mezani na kufurahia chakula, unaweza kweli kuwa na furaha huku ukijua kwamba kuna familia nyingine zinazolala na njaa ya haki, zikiomboleza wapendwa wao?
Kwa JAJI: Je, unafahamu kwamba kalamu yako inaweza kuwa na nguvu kuliko silaha? Hukumu yako inaweza kumrudishia mtu uhuru au kumfungia gerezani bila haki. Usisahau kwamba joho la mahakama si kinga dhidi ya hukumu ya dhamiri na historia.
Kwa POLISI: Je, unakumbuka kwamba silaha uliyopewa ni kwa ajili ya kulinda maisha, si kuyakatisha? Sare yako ni ishara ya dhamana ya kulinda raia, si ruhusa ya kuwatesa, kuwatesa kisaikolojia, kuwateka au kuwapoteza watu.
Kwa WENYE MAMLAKA: Je, mnaelewa kwamba madaraka ni dhamana, si umiliki wa maisha ya wengine? Cheo chako ni cha muda. Uhai wa mwanadamu una thamani isiyopimika. Hakuna cheo kinachokupa haki ya kuamua kwamba maisha ya mwingine hayana thamani.
Nataka kila mwenye mamlaka aelewe jambo moja:
Unaweza kujenga nyumba yenye geti kubwa, ukuta mrefu na kamera za usalama. Unaweza kununua gari lenye vioo visivyoonekana kutoka nje. Unaweza kuzungukwa na walinzi na kuishi kwenye mazingira ya kifahari.
Lakini huwezi kujenga ukuta wa kutosha kuzuia dhamiri yako isikuulize maswali.
Unaweza kuificha kweli kwa muda, unaweza kuzuia watu wasizungumze, unaweza kutumia mamlaka kuzuia ushahidi usisikike, lakini huwezi kuufuta ukweli katika kumbukumbu za historia.
Kumbuka: Watoto wako hawahitaji urithi wa nyumba na magari pekee; wanahitaji urithi wa jina lenye heshima. Usimwachie mtoto wako mali ambayo siku moja ataionea aibu kuitaja.
Mali inaweza kurithishwa. Cheo kinaweza kurithishwa kwa kumbukumbu. Lakini wajibu wa kujibu mbele ya historia hauhamishwi kwa watoto wako.
Mithali 21:3 inasema:
“Kutenda haki na hukumu humpendeza BWANA kuliko kutoa sadaka.”
Na Yakobo 3:1 inatukumbusha kwamba wanaofundisha na kuongoza wengine watapata hukumu iliyo kubwa zaidi.
SWALI LA MWISHO
Siku moja utastaafu. Utavua sare. Utaliacha joho la mahakama. Utakabidhi ofisi. Utashuka kwenye gari la Serikali. Walinzi watarudi makwao.
Utabaki wewe, familia yako na dhamiri yako.
Je, utaweza kukaa na wajukuu zako, ukiwaangalia machoni na kuwaambia kwamba ulitumia mamlaka yako kulinda haki, utu na uhai wa mwanadamu?
Au utakuwa na nyumba kubwa, magari mazuri na akaunti zilizojaa fedha, lakini historia yako imejaa majina ya watu ambao hawakupata haki?
USIWE TAJIRI WA MALI KWA KUMFANYA MWINGINE KUWA MASKINI WA HAKI.
Mamlaka ni ya muda. Mali ni ya muda. Cheo ni cha muda.
Lakini madhara ya dhuluma yanaweza kurithiwa na vizazi, na kumbukumbu ya jinsi ulivyomtendea mwanadamu mwenzako inaweza kuishi muda mrefu kuliko maisha yako.
Usiogope tu kupoteza cheo. Ogopa kupoteza utu wako ukiwa bado unacho.
Necto Kitiga retweeted
Mwanamuziki, Afande Sele amepigwa stop kuendelea kutumbuiza kwenye tamasha la Miaka 30 ya Bongo Fleva kutokana na hatua yake ya kuzungumzia na kuwakumbuka watu waliotangulia mbele za haki kwa kuuwawa wakati wa matukio ya kikatili ya Oktoba 29, 2025.
Necto Kitiga retweeted
Ni week ya 3 leo (Siku 21) tangu kutekwa kwa ndugu yetu Twaha Mwaipaya.
Bado tunaendelea kusema #FreeTwahaMwaipaya























