GASTON SHUNDO GARUBINDI (@ShundoGaston) header
GASTON SHUNDO GARUBINDI (@ShundoGaston) profile picture

SENIOR ADVOCATE | CHADEMA CC MEMBER 2019-2024 | CHADEMA DIRECTOR FOR LEGAL AND HUMAN RIGHT 2024-2029.

Dar es Salaam, Tanzania
Joined February 2019
Photo by GASTON SHUNDO GARUBINDI (@ShundoGaston)Photo by GASTON SHUNDO GARUBINDI (@ShundoGaston)Photo by GASTON SHUNDO GARUBINDI (@ShundoGaston)Photo by GASTON SHUNDO GARUBINDI (@ShundoGaston)Photo by GASTON SHUNDO GARUBINDI (@ShundoGaston)Photo by GASTON SHUNDO GARUBINDI (@ShundoGaston)Photo by GASTON SHUNDO GARUBINDI (@ShundoGaston)Photo by GASTON SHUNDO GARUBINDI (@ShundoGaston)Photo by GASTON SHUNDO GARUBINDI (@ShundoGaston)Photo by GASTON SHUNDO GARUBINDI (@ShundoGaston)
Nimetoka Gereza la Ukonga, kumtembelea Mhe Tundu Antiphas Mghwai Lissu mfungwa mwenye namba 623/2026, yuko salama ameanza maisha mapya. Mhe lissu ametupatia ridhaa Mawakili wa Chama, chini ya Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Dr Rugemeleza Nshalla kumwakilisha kwenye rufaa inayokusudiwa kusajiliwa na mambo yote yanayohusiana nayo, kufuatia uamuzi uliotolewa tarehe 6 November 2026 na Mahakama kuu, Masijala ya Dar Es Salaam. Mhe Lissu amepokea nakala ya taarifa ya kukata Rufaa (Notice of Appeal) ambayo imesajiliwa Mahakamani, pamoja na nakala ya hukumu iliyosomwa November 06, 2026. Aidha, hatua nyingine za kisheria zinaendelea kwa uratibu wa mawakili wake.
42
291
6
1,172
29,708
TAARIFA YA KESI YA ATHUMAN JOSEPH KAZINZA - KATIBU MWENEZI (W) BUSEGA Kesho tarehe 9/11/2026 saa 3:00 kamili asubuhi Mahakama ya Hakimu Mkaazi Mkoa wa Simiyu itaanza kusikiliza kesi ya jinai Na. 15461/2026 Jamhuri dhidi ya Athuman Joseph Kazinza anayeshitakiwa kwa kosa la UCHOCHEZI kinyume na Kifungu cha 390 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16 rejeo la 2023. Miongoni mwa mashahidi wa Jamhuri katika kesi hiyo ni pamoja na Mkuu wa upelelezi (RCO) Mkoa wa Simiyu na Mkuu wa upelelezi (OC CID) Wilaya ya Busenga. Nitoe wito kwa viongozi wote na wanachama na wapenda haki wote ndani ya Mkoa wa Simiyu, Mikoa na Wilaya, Kanda ya Serengeti kesho asubuhi tufike Mahakamani kumpa supporti na kumpa nguvu Kamanda Athumani Joseph Kazinza. Nguvu yetu katika kupigania haki na ustawi wa demokrasia ni umoja na mshikamano pale mmoja wetu anapokuwa na kesi kama anapambana nayo Kazinza. Mtuhumiwa atatetewa na Mawakili wa Chama, Alex Dotto Massaba na Wakili Alloyce Osewe Kajitamus.
4
48
161
3,646
GASTON SHUNDO GARUBINDI retweeted
6.11.2026: Hukumu ya TUNDU LISSU NA KUMBUKUMBU YA KESI YA MWALIMU NYERERE YA MWAKA 1958. HISTORIA INATUFUNDISHA NINI? Leo, tarehe 6 Novemba 2026, Tundu Lissu ameshinda kesi ya uhaini lakini mahakama ikasema amepatikana na hatia ya uchochezi (incitement) na kuhukumiwa kifungo cha miaka 4. Tunamshukuru Mungu kwa kesi ya uhaini kutupiliwa mbali na kumpongeza Lissu kwa umahiri na ujasiri wake hadi kujitetea. Lakini hukumu ya uchochezi inasikitisha, inafikirisha na inatukumbusha historia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, ambaye naye mwaka 1958 alikutwa na hatia ya jinai ya kashfa (criminal libel) wakati wa harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika. Makosa haya mawili ni tofauti kisheria, lakini kesi hizi zinafanana katika jambo muhimu: zote zilihusu kiongozi mkuu wa upinzani aliyeshtakiwa na Serikali kutokana na kauli zake za kisiasa. Turejee historia. Tarehe 27 Mei 1958, Mwalimu Nyerere alichapisha makala katika gazeti la Sauti ya TANU, Toleo Na. 29, akiwakosoa Wakuu wawili wa Wilaya wa Serikali ya kikoloni kwa madai ya kutumia madaraka yao vibaya na kuihujumu TANU. Akafunguliwa kesi ya jinai Na. 2207/1958 chini ya kifungu cha 187 cha Kanuni ya Adhabu (Penal Code). Serikali ya Uingereza ilitoa maelezo kuhusu mashtaka hayo katika Bunge lake (House of Commons) tarehe 26 Juni 1958. Nyaraka za UN zinathibitisha kwamba Mwalimu alikutwa na hatia katika mashtaka mawili na kuhukumiwa kulipa faini ya shilingi 3,000 za Afrika Mashariki, sawa na pauni 150 za wakati huo, au kifungo cha miezi sita. Alilipa faini tarehe 12 Agosti 1958 na hakukata rufaa. Kesi hiyo ilizua mjadala mkubwa. Wanaharakati wa kupigania uhuru huko London walihoji iwapo Mwalimu angepata haki katika mahakama za kikoloni na kudai kuwepo kwa waangalizi huru. Serikali ilikataa, ikisisitiza kuwa uamuzi wa kufungua mashtaka ulikuwa chini ya mamlaka ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Miaka 68 baadaye, tunajikuta tena tukitafakari maswali kuhusu uhuru wa kisiasa, matumizi ya sheria za jinai na nafasi ya mahakama katika mfumo wa kidemokrasia. Pamoja na hukumu ya mwaka 1958, Mwalimu Nyerere aliendelea na harakati zake hadi Tanganyika ilipopata uhuru mwaka 1961. Funzo muhimu ni kwamba hukumu ya jinai dhidi ya kiongozi wa kisiasa si lazima iwe mwisho wa safari yake ya kisiasa. Historia inaonesha umuhimu wa kuendeleza majadiliano (dialogue) badala ya mapambano na vurugu (confrontation). Kwa wanaothamini demokrasia, mfumo wa vyama vingi, haki za binadamu, uhuru wa kujieleza na utawala wa sheria, hukumu ya uchochezi dhidi ya kiongozi mkuu wa upinzani inaibua maswali mazito yanayohitaji mjadala mpana wa kitaifa. Je, mipaka kati ya ukosoaji halali wa Serikali na uchochezi wa jinai ikoje? Je, mwanasiasa awe mpinzani au wa chama tawala atakosoa je Serikali au kudai maboresho au mageuzi bila kuhofia kutafsiriwa kuwa mchochezi? Je, wananchi watawezaje kudai haki zao kwa nguvu ya hoja bila kuonekana wanachochea uvunjifu wa amani? Walimu na wanataaluma tutawezaje kufundisha, kuchambua sera, kutoa mapendekezo na kukosoa mifumo ya utawala bila kuhofu kuitwa wachochezi? Viongozi wetu wa dini watawezaje kutekeleza wajibu wao wa kinabii wa kukemea maovu na kusimamia haki bila kuonekana wanachochea waumini wao? Uhuru wa kujieleza una mipaka yake na hauhalalishi haki ya kukashfu, kuchochea vurugu au uhalifu. Lakini ni muhimu sana kuweka mipaka iliyo wazi kati ya uchochezi wa jinai na ukosoaji halali wa kisiasa. Iwapo sheria za jinai zitatumika kudhibiti ukosoaji halali wa kisiasa au kitaalamu, tunaweza kujikuta tunadhoofisha demokrasia, haki za binadamu, kuongeza hofu na kuzidisha mkwamo wa kisiasa na kiuchumi badala ya kuutatua. Hukumu ya leo inatupa sababu nyingine ya kujadili kwa kina uhuru wa kujieleza, uhuru wa mahakama, haki za raia na za vyama vya upinzani na mipaka ya matumizi ya sheria za jinai katika siasa. Ninarejea msisitizo wangu wa muda mrefu kuhusu falsafa ya Rais Samia ya 4Rs. Tujenge utamaduni wa kusikilizana na kukosoana kwa hoja TUJISAHIHISHE
61
364
14
1,082
29,657
MAHAKAMA YAKATAA MAPINGAMIZI KESI YA MWENYEKITI BAVICHA MKOA WA KIGOMA - KESI KUSIKILIZWA IJUMAA: Kesi ya Habeous Corpus iliyofunguliwa na mawakili wanao mwakilisha mwenyekiti wa Bavicha mkoa wa Kigoma , Coletha Clavery Ntidyicha imeendelea leo mahakama kuu, masijala ya Dar es salaam kwa hatua ya kusikiliza mapingamizi yaliyoletwa na Jamhuri. Mahakama baada ya kusikiliza pande zote, imetupilia mbali pingamizi hilo na kuelekeza maombi ya msingi yasikilizwe tarehe 30-10-2026. Hata hivyo, mawakili wa mleta maombi wamepewa ruhusa ya kuleta kiapo cha nyongeza leo ambapo upande wa Jamhuri watapaswa kuleta majibu dhidi ya kiapo hicho kesho na keshokutwa maombi yatasikilizwa. Coletha alikamatwa na Jeshi la Polisi ambapo linamshikilia kinyume na matakwa ya kifungu cha 134(1),(2) na (4) cha sheria ya Mwenendo wa makosa ya jinai, sura ya 20 urekebu wa mwaka 2023. Katika maombi hayo, mawakili wa mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Kigoma, Coletha wanaiomba Mahakama kuwatala mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Mkurugenzi wa makosa ya Jinai, Mkuu wa kituo cha Polisi Chang’ombe, RPC, RCO Temeke kufika mahakamani kueleza sababu za kuendelea kumshilia Coletha kinyume na sheria za nchi hii. Kesi ya Coletha ni moja ya kesi 9 za maombi ya Habeous ambazo ziko Mahakama mbalimbali. Nawashukuru mawakili @Advocate_Jebra , @MahinyilaD , @Advocate_Kisabo , Nicholaus mvano na wakili @AdvMatata kwa msaada wenu, Mungu awabariki sana!
48
131
2,658
John Justine Pambalu , Mkurugenzi wa Organization na mafunzo amefikishwa mahakamani leo kisutu na kusomewa kosa la Uhaini.
12
51
2
172
4,871
Jeshi la Polisi wilaya ya Kahama linamshikilia Katibu wa Kanda ya Victoria Zacharia Obad baada ya kuvamia nyumbani kwake jana usiku majira ya saa nane kwa tuhuma ambazo bado hazijajulikana. Kwa sasa, Zacharia Obad yupo kituo cha Polisi Kahama, akisubiri kuchukuliwa maelezo. Wakili Alex Dotto Massaba yupo mjini Kahama kutoa msaada wa kisheria kwa Obad. Obad Zacharia ni kiongozi mkubwa, angeitwa Polisi kama wanashida naye angefika kuliko kutumia utaratibu wa kuvamia makazi yake Kahama mjini usiku wa manane na kusababisha taharuki. Obad zqcharia anakuwa mwanachama wa tano, kukamatwa ndani ya kipindi kifupi. Wengine waliokamatwa na Polisi ni Mkurugenzi wa Organization na Mafunzo John Justine Pambalu, aliyekamatwa Arusha na kusafurishwa hadi Dar. Wengine ni Mwenyekiti Bavicha Mkoa wa Kigoma Coletha Ntidyicha aliyekamatwa Dar Es Salaam, Mwenyekiti wa Bavicha kanda ya Victoria Fred Masele, aliyekamatwa Mwanza , Edson Malyo Mliyinga huyu alikamatwa mkoani Iringa, Fadhili Benedict Mbeya alikamatwa Dar Es salaam na Doris Msigwa aliyekamatwa Arusha. Tafadhali, watuhumiwa hawa wafikishwe Mahakamani kwa mujibu wa sheria za nchi yetu.
38
98
2,176
Kazi nzuri ya Baraza la Wanawake CHADEMA. Chama hiki tutakilinda kwa wivu mkubwa.
43
202
1,587
Inaonekana kuna mkakati wa kukamata viongozi wa Baraza la Vijana Nchi hii. Tayari mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Kigoma Coletha Clavery Ntidyicha na Mwenyekiti wa vijananKanda ya victoria wamekamatwa. Tanzania ni moja ya nchi zilizoridhia mkataba wa haki za kiraia na kisiasa, ni bahati mbaya kwamba, sasa hivi matendo ya kisiasa yanageuzwa kuwa makosa ya jinai na washindani walioshindwa kwenye majukwaa ya kisiasa.
3
73
2
215
5,259
CHADEMA KICHEKO MAHAKAMA KUU DHIDI YA JAMHURI: Kuanzia tarehe 09 October 2026 hadi leo ijumaa ya tarehe 16 October 2026 jumla ya kesi 03, zinazowahusisha chadema zimetolewa uamuzi na Mahakama kuu ya Tanzania masijala mbalimbali huku chadema wakiibuka kidedea. 1. MHAKAMA KUU - MASIJALA YA MORORGORO. October 09, 2026 Mahakama kuu masijala ya Morogoro ilikubali maombi Criminal Revision No. 12322/2026 baina ya LUCIA SIMON SHAYO VRS REPUBLIC. Katika Maombi hayo, mawakili wa CHADEMA waliomba Mahakama kuu iangalie uhalali wa mwenendo na amri za Mahakama ya wilaya ya Morogoro iliyokubali taarifa ya mawakili wa Jamhuri kuongeza orodha ya mashahidi na vielelezo kwenye kesi inayomkabili mwanachama wa chadema , Lucia Simon Shayo. Katika uamuzi wake, Mhe Jaji Ebrahim Rose aliona maombi ya mawakili wa Lucia Simon Shayo yana mashiko na alikubali kuwa taarifa ya kutumia vielelezo vya Jamhuri havikufuata sheria na kwamba taarifa yake ilikuwa unreasonable na hivyo akatumia mamlaka yake kufuta taarifa (notice) hiyo. Kwa kufutwa taarifa hiyo, mashahidi na vielelezo hivyo havitakuwa sehemu ya ushahidi wa kesi Jamhuri dhidi ya Lucia Simon Shayo. 2. MAHAKAMA KUU - MUSOMA Tarehe 16/10/2026 Mahakama kuu Masijala ya Musoma imetoa uamuzi kufuatia Rufaa ya mawakili wa Chadema dhidi ya uamuazi wa Mahakama ya wilaya ya Bunda iliyomtia hatiani Mwanachama mmoja maarufu kama Tolu kupitia shauri “Criminal Appeal No. 13554/2026 GEORGE MAPULI BUKINGI VRS REPUBLIC”. Bukingi ni mwanachama pekee aliyepatikana na hatia kwenye kesi ya wananchi 30 walishitakiwa kufuatia vurugu za October 29, 2025. Hata hivyo Mawakiki wa Chadema walikata Rufaa mahakama kuu na leo, Mhe Jaji E Kakolaki amekubaliana na hoja za mawakili kwamba ushahidi uliotolewa na upande wa serikali wakati wa usikilizwaji wa kesi haukujitosgeleza kumtia hatiani ndugu Bukingi. Hivyo Mahakama imekubali rufaa na kuelekeza aachiwe mara moja, ameshaachiwa tayari, ameungana na familia yake Bunda Mjini. 3. DAR ES SALAAM Hatimaye uamuzi wa shauri namba 7300/2026 lililofunguliwa mawakili wa Mhe Tundu Lissu kupinga kitemdo cha uongozi wa Gereza la Ukonga kuwazuia mawakili kuongea na mteja wao Mhe Lissu bila kusikikizwa na Maafisa wa Magereza umetolewa. Jopo la Majaji watatu wamekubali kwamba kitendo kilichofanywa na Magereza Ukonga ni kinyume na sheria na Mahakama imeelekeza utaraibu ufuatwe. Ushindi huu ni ushindi mhimu dhidi ya uhuru wa mawakili katika kutekeleza majukumu yao ya uwakili lakini pia ushindi huu umeifahamisha dunia namna Mamlaka zinavyomtendea isivyo haki Mhe Tundu Lissu kwa kumnyika nafasi ya kuzungumzq na mawakili wake. Kwa upande wa Mahakama, Jamhuri wameshindwa katika mashauri yote matatu. Mapambano yanaendelea Mahakamani. Nawashukuru kwa dhati Mawakili waliojitolea nankupigania ushindi wa mashauri haya, taasisi za kiraia, wananchi ambao mumefuatilia na kuwapatia maneno ya faraja wapambanaji wetu Mahakamani, Mungu awabariki sana! Tumehitimisha week hii Mahakamani kwa kishindo kikubwa!
6
34
1
139
5,503
Jana mahojiano hayakukamilika hivyo, Polisi walipanga leo kuendelea kumhoji Mhe John Pambalu, Mkurugenzi wa Organisation na Mafunzo. Yatakapokamilika tutawataarifu kilichojili.
5
46
275
4,044
MAHAKAMA KUU MUSOMA YAMWACHIA GEORGE MAPULI BUKINGI: Mahakama kuu ya Tanzania, masijala ya Musoma imekubali rufaa ya George Mapuli Bukingi aliyetiwa hatiani na mahakama ya wilaya ya Bunda. George Bukingi ni miongoni mwa vijana walioshitakiwa kutokana na vurugu za October 29, 2026 na kupewa kesi ya uhaini na baadaye ikabadilishwa na akashitakiwa kwa kosa la kumjeruhi Askari Polisi. Mahakama ya wilaya ya Bunda ilimhukumu Bukingi kifungo cha miaka 5, ikidai kwamva Mahakama iliridhika na ushahidi uliotolewa wakati wa usikilizwaji wa kesi . Hata hivyo, mawakili wa CHADEMA hawakuridhika na uamuzi wa Mahakama ya wilaya Bunda na wakaamua kukata rufaa Mahakama kuu - Musoma. Leo Mahakama kuu masijala ya Musoma, Mhe Jaji Kakolaki ametoa uamuzi. Katika uamuzi wake, Mhe Jaji Kakolaki amekubali hoja za warufani kwamba ushahidi haukijitosheleza kumtia hatiani na hivyo mahakama imemuachia rasmi leo. Kuachiwa kwa Bukingi, kumefanya watuhumiwa wote 30 walioshitakiwa kwa makosa ya uchaguzi wa october 29, Wilayani Bunda kuwa huru. Nawashukuru mawakili Alex Massaba nq Aloyce Kajitamusi kwa kuwa sehemu ya kutetea haki ya George Mapuli. Asanteni Bunda kwa ushirikiano kwa kipindi chote cha kushughulika na kesi ya Kaunya nanwenzake 29.
18
83
1
258
8,497
Mkurugenzi wa Organization na Mafunzo @John_Pambalu amefikishwa Central Police Dar Es Salaam. Kwa sasa Mawakili wetu @Advocate_Jebra na @mwasipu_hekima wanakwenda Central Police ili aweze kuchykuliwa maelezo. Taarifa zaidi kuhusu amehojiwa kitu gani tutawataarifu baadaye! @MariaSTsehai @Liberatus80 @HecheJohn @JohnKitokavo08 @HildaNewton21 @jjmnyika @bavicha_taifa @BrendaRupia
3
55
3
183
5,734
UAMUZI KESI YA SAID ISSA UMESOGEZWA MBELE. Pokeeni taarifa kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam kwamba, Mahakama imeahirisha kutoa Uamuzi juu ya Maombi ya zuio katika Maombi Madogo Namba 14864 ya 2026 baina ya Said Issa Mohamed & Ahmed Rashid Khamis dhidi ya Registered Trustees of Chama cha Demokrasia na Maendeleo & Secretary General of Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)hadi tarehe 22/10/2026 saa 8 Mchana. Sababu za ahilisho hilo ni kutokana na Mhe Jaji aliyetarajiwa kutoa uamuzi huo kuwa na majukumu mengine nje ya kituo cha kazi. Tunawashukuru wanachama kwa utayari wao wa kufika Mahakamani, kwa taarifa hii, Tunaomba sasa tukutane Mahakamani tarehe 22/10/2026 saa nane mchana.
4
35
1
109
2,775
MAHAKAMA KUU KUTOA UAMUZI KESHO KESI YA MAOMBI YA SAID ISSA MOHAMED DHIDI YA CHADEMA. Kesho tarehe 8 Oktoba 2026 Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam itatoa Uamuzi juu ya Maombi ya Zuio katika Maombi Madogo Namba 14864 ya 2026 baina ya Said Issa Mohamed & Ahmed Rashid Khamis dhidi ya Registered Trustees of Chama cha Demokrasia na Maendeleo & Secretary General of Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mnamo saa 8 na Nusu Mchana. Wanachama na viongozi mnaombwa kufika kwa wingi kusikiliza uamuzi huo. Haya ni maombi mengine ambapo waombaji wanaomba Mahakama kuu kufungia Chama kwa Mara nyingine tena.
3
39
119
3,231
Leo viongozi na wanachama 17 wakiongozwa na Katibu wa Kanda ya Serengeti Jackson Rashid Mnyawami wamepandishwa kizimbani, Mahakama ya Hakimu mkazi wa Mkoa wa Shinyanga dhidi ya mashitaka ya Ugaidi yanayowakabili. Mashauri ya leo ni pamoja na Economic case namba 16506/2026 inayomkabili Jackson Rashid Mnyawami, Mashauri mengine ni Economic Case No. 16503/2026, inayomkabili Jackson Venant Kabyeseleza, Economic Case No. 16504/2026 Inayomkabili Edwin Otieno Ongito na wenzake 8, Economic Case No. 16505/2026, inayomkabili Daniel Emanuel Athuman , Economic case namba 16506/2026 inayomkabili Laurent na wenzake 4.
2
48
175
3,886
Makamu mwenyekiti Bara @HecheJohn aliwasili kwenye mkutano wa hadhara jana pale Bunda kwa hamasa hiyo. Kazi ya Bunda ilikuwa nzuri.
19
98
1,077
KESI ZA LEO SEPTEMBER 25, 2026 DHIDI YA WANACHAMA NA VIONGOZI WA CHADEMA NCHINI: September 25, viongozi wenzetu na wanachama watakuwa na mashauri yafuatayo kwenye mahakama mbalimbali hapa nchini. 1. Dsm, criminal session No 19605/2026 shauri la Uhaini dhidi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mhe Lissu litaendelea ambapo Mhe Lissu anaendelea na kuwasilisha majumuisho ya hoja za mwisho. 2. Mkoani Morogoro, mwanachama Lucy simon shayo atakuwa mahakama kuu kwenye shauri la marejeo namba 12322/2026 ambalo litakuja kwa hatua ya kusomwa uamuzi. 3. Mkoani Shinyanga, Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Shinyanga itataja shauri namba 16506/2026, Jamhuri dhidi ya Jackson Rashid Mnyawami. (Ikumbukwe kuwa Jackson Mnyawami ni Katibu wa Chadema Kanda ya Serengeti ) Mashauri mengine (04) yatakayotajwa leo dhidi ya wanachama ni pamoja na shauri namba 16503/2926 Jamhuri dhidi ya Jackson Venant Kabyeseleza, Shauri Na. 16505 Jamhuri dhidi ya Daniel Emanuel Athuman, Shauri Na. 16504/2026 Edwin Otieno Ongito na wenzake 8 na shauri namba 16506/2026 Jamhuri dhidi ya Godwine Laurent na wenzake 4. Ukiacha Lucy Shayo, watuhumiwa wengine wote wanaletwa mahakamani wakitokea Magereza kwa kuwa makosa waliyopewa hayana dhamana kisheria. Viongozi na wanachama waliopandishwa kizimbani leo ni 19.
1
40
1
126
3,192
Orodha hii ni kesi kuanzisa kesho jumatatu tarehe 21 hadi Ijumaa tarehe 25/09/2026. Kila mwisho wa week nitakuwa naweka hapa orodha ya kesi dhidi ya viongozi ma wanachama wa CHADEMA zinazotarajiwa kuendelea Mahakamani nchini nzima. Ukiona kuna kesi dhidi ya kamanda wetu eneo lako, panga siku hiyo kuungana naye mahakamani, njoo Mahakamani uoneshe solidarity.
3
77
1
212
4,920
KESI DHIDI YA VIONGOZI NA WANACHAMA LEO TAREHE 16-09-2026: 1. Kesi ya uhaini dhidi ya Mhe Lissu, Criminal session no 19605/2026 inaendelea Mahakama kuu Dar es salaam. 2. Mahakma ya wilaya Ilala, kesi ya ugaidi inayomkabili Athumani Abdallah Muganda itatajwa. 3. Mbeya, kesi namba 16394/2026 Noah mwalwange na wenzake 3 itatajwa. 4. Kesi namba 16393/2026 Jamhuri dhidi ya Jasiri Robert Mwaisumbi nayo itatajwa.
3
35
127
2,467