Serikali ya Peru iliteketeza tani 10.7 za dawa za kulevya zilizokamatwa, kulingana na taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo siku ya Ijumaa, tarehe 27 Novemba, 2026 jijini Lima.
Dawa hizo za kulevya zilikamatwa na Kurugenzi ya Kupambana na Dawa za Kulevya ya Polisi ya Peru (PNP) pamoja na vitengo vingine katika operesheni mbalimbali.
113
Baada ya kumalizana mbele ya Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) hivi karibuni, Morocco na Senegal sasa zitahamia Lagos, nchini Nigeria wakati zitakapokuwa zinawania tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka 2026 , ambaye anatarajiwa kujulikana Disemba 2, 2026.
Wanaopigiwa chapuo kushinda tuzo hiyo, ni pamoja na Achraf Hakimi, Brahim Díaz na Ismael Saibari, wote kutoka Morocco, huku Sadio Mané na Pape Gueye, wakiwania tuzo hiyo kwa upande wa Senegal.
Unadhani nani anastahili tuzo hiyo kati ya wachezaji hawa?
133
Taasisi ya Madaktari Wasio na Mipaka (MSF), wamelaani shambulio lililoua la Israel, lililoua wafanyakazi wake wawili, katika kliniki moja huko Gaza.
MSF imetaka uwajibikaji baada ya shambulio hilo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan, azungumza katika Jukwaa la Al Sharq 2026 jijini Istanbul:
1
259
Waziri Fidan:
- Muungano wa Makka utakuwa jumuishi zaidi kwa kushirikisha nchi zingine za kikanda
- Ushirikiano lazima upanuke zaidi ya usalama ili kujumuisha ujumuishaji wa kiuchumi
- Utulivu pekee hautoshi; lengo ni utaratibu na uwakilishi jumuishi wa kikanda
1
16
Waziri Fidan:
- Palestina inabaki kuwa dira yetu kuu ya maadili
- Lazima tuongoze juhudi za kutoa misaada ya kibinadamu, kujenga upya Gaza na kutetea sababu ya Palestina hadi uhuru na haki itakapotawala
- Tunafanya kazi bila kuchoka leo na hatutarudi nyuma hadi amani ya haki na ya kudumu itakapopatikana
- Kwamba amani inawezekana tu kupitia suluhisho la mataifa mawili na taifa huru la Palestina, huku Jerusalem Mashariki ikiwa mji mkuu wake
22
Kundi la majambazi waliokuwa na silaha, walivamia gari moja lililokuwa limebeba dhahabu, kisha kuwamiminia risasi waliokuwemo ndani ya gari hilo, kabla ya kutokomea na vito hivyo, katika tukio lililotokea Novemba 27, 2026, katika eneo la Callao nchini Peru.
Kulingana na afisa mwandamizi wa polisi katika eneo hilo, kundi lilikuwa na jumla ta watu 10 ambao walitumia magari matatu, kutekeleza uhalifu huo.
Watu wawili waliokuwemo ndani ya gari hilo lenye dhahabu, akiwemo raia mmoja wa India, walijeruhiwa na kwa sasa wanapokea matibabu.
2
234
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan baada ya mkutano uliofanyika mjini Islamabad kama sehemu ya Muungano wa Ulinzi wa Makka:
-Muungano huu unapiga hatua katika kuimarisha taasisi na kuanza kazi
-Maamuzi yamekubaliwa kimsingi kuhusu kuwa na Katibu Mkuu raia na Kamandi ya pamoja ya Kijeshi
-Muungano huo pia ulijadili tishio la wapiganaji wa Houthi linalowakabili Saudi Arabia na yanayojiri katika Ghuba
-Mataifa wanachama yanalenga kuleta pamoja uwezo wao wa kijeshi na sekta ya ulinzi ili kuimarisha mchango wao kwa amani na usalama katika kanda
-Uturuki itakuwa mwenyeji wa mkutano wa kamati unaofuata
- Majadiliano pia yaliangazia mchakato wa uanachama kwa nchi zinazotaka kujiunga na muungano huo
1
184
Wizara ya Mambo ya Nje ya Pakistan kuhusu mkutano wa muungano wa ulinzi wa Makka uliofanyika mjini Islamabad:
- Ulisisitiza mataifa ya Uturuki, Saudi Arabia na Pakistan kuendelea kufanya kazi pamoja kwa lengo la amani katika kanda, usalama
- Pakistan, Uturuki, Saudi Arabia walisisitiza dhamira yao kwa misingi, malengo ya makubaliano
- Nchi zote tatu zililaani kwa pamoja mashambulizi ya wapiganaji wa Houthi yanayolenga raia na miundombinu nchini Saudi Arabia
1
171
Morocco na Senegal huenda wakakabiliana tena wakati mataifa hayo mawili yanapojiandaa kwa michuano ya Soka la Ufukweni ya CAF nchini Senegal, siku chache baada ya uamuzi muhimu uliowarudishia Senegal kombe lao la AFCON 2025.
Mashindano ya soka la ufukweni yanaanza Jumamosi, tarehe 28 Novemba katika eneo la pwani la Saly, huku Senegal wakitafuta ubingwa wa taji hilo kwa mara ya sita mfululizo na Morocco wakitaka kulinyanyua kwa mara ya kwanza.
Pande zote mbili ziko katika makundi tofauti, hivyo hawawezi kukutana katika hatua ya makundi. Lakini kama wote watamaliza miongoni mwa timu mbili bora hatua hiyo, wanaweza wakakabiliana katika nusu fainali tarehe 4 Disemba au hata katika fainali tarehe 6 Disemba.
1
163
Afisa mwandamizi wa ujasusi wa wapiganaji wa RSF ametangaza kuunga mkono jeshi la Sudan na kushtumu uongozi wa kundi hilo kwa kuangalia maslahi yao binafisi na ya mataifa ya nje.
Katika video iliyosambazwa na vyombo vya habari vya Sudan na wanaharakati siku ya Ijumaa, Brigedia Jenerali Dahiya Hamdan al-Tahir amejitambulisha kama mkuu wa oparesheni maalum za kijasusi za RSF jimbo la Kati la Darfur na mwanachama wa kusajili wanaojiunga na kundi hilo.
Amesema yuko tayari kuijunga na jeshi na vikosi washirika katika vita dhidi ya wapiganaji wa RSF.
1
164
Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki imetaka maelezo kutoka kwa Balozi wa Georgia nchini Uturuki Archil Kalandia, kulingana na vyanzo vya wizara:
- Uturuki imeeleza kuhusu matukio ya wakati wa mechi ya Ligi ya UEFA ya Europa ya Besiktas eneo la Batumi
- Wizara pia ilitoa ushahidi kuhusu matukio hayo na kutaka uchunguzi wa kina kufanyika
- Inasema kuwa utaratibu wa kisheria unatakiwa kuanzishwa dhidi ya wale waliotumia nguvu zaidi ya inavyotakiwa kwa raia wa Uturuki
166
Jeshi la Uganda siku ya Ijumaa lilisema linapanga kuondoa vikosi vyake kutoka mji muhimu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kushtumu wapiganaji wanaodaiwa kuunga mkono serikali kwa kuendeleza mashambulizi mashariki mwa nchi.
Tangazo hilo la Uganda linakuja siku kadhaa baada ya DRC kusema kuwa imemtaka balozi wa Uganda kutoa ufafanuzi kuhusu ujumbe uliotolewa na mkuu wa majeshi ya Uganda.
Eneo la mashariki mwa DRC lenye utajiri wa madini limekuwa likikabiliwa na mapigano kwa zaidi ya miaka 30.
Wanajeshi wa Uganda wako katika mikoa ya Ituri na Kivu Kaskazini kwenye mpaka wa DRC na Uganda tangu 2021.
125
Kama ulikuwa mpenzi wa Ligi Kuu ya mpira wa kikapu Marekani (NBA) basi utakuwa unamfahamu mwamba aliyevuma miaka ya themanini na tisini Hakeem Abdul Olajuwon.
Mzaliwa huyu wa pale mjini Lagos nchini Nigeria alipewa jina la utani la ‘’the Dream’’ na alicheza NBA misimu 18.
Rais wa Kenya, William Ruto, amemkosoa vikali aliyekuwa Naibu Rais, Rigathi Gachagua, akipuuza madai ya ushawishi wake katika eneo la Mlima Kenya, anakotoka Gachagua, huku akisisitiza kuwa wananchi ndio wenye uamuzi wa mwisho katika kuchagua viongozi wao.
Akizungumza Kaunti ya Kiambu, katikati mwa Kenya siku ya Ijumaa, Rais Ruto aliwahimiza wakazi kuwapima viongozi kulingana na utendaji wao badala ya muonekano au maneno ya kisiasa.
Ni nyinyi ndo mnachagua Rais? Wakati mnachagua kiongozi mnampima na sura ama kazi? Na makelele ama kazi? Kila mtu anapimwa na kazi yake. Nyinyi ndo mnaamua ama kuna mtu amewabebea kura zenu? Mnabebewa akili ama kila mtu ako na akili yake?” aliuliza.
“Kuna mtu ananiambia ati kama nataka kura za Lari na Kiambu lazima niende nipige magoti kwake. Niende nipige magoti kwa nyumba ya mtu ama niongee na nyinyi?”
134
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amesema uchumi wa nchi yake umeimarika na sasa nchi hiyo inaweza kufanya biashara na nchi nyengine.
Rais Mnangagwa alikuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari wa Kenya alipokuwa kwenye ziara rasmi nchini Kenya Novemba 27, 2026.
Utetezi wa Mnangagwa unakuja huku kukiwa na mageuzi ya kiuchumi katika kipindi cha mwaka 2026 baada ya kuanzishwa kwa sarafu ya Dhahabu ya Zimbabwe (ZiG) Aprili 2024, inayoungwa mkono na dhahabu.
Kufikia Novemba 2026, vikwazo vingi vya nchi za Magharibi dhidi ya Zimbabwe zimeondolewa, na kubaki vile vya watu binafsi, vikwazo vya silaha vya EU, na vikwazo vya kisheria vya Marekani kuhusu mikopo ya kimataifa.
Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), na wakuu wa nchi binafsi wamekuwa wakiitetea nchi hiyo na kutaka kuondolewa mara moja kwa vikwazo bila masharti.
134
Uturuki na Urusi zimethibitisha lengo lao la kuongeza mara mbili kiwango cha biashara kutoka Dola bilioni 50 hadi kufikia Dola bilioni 100 huku mawaziri wakisaini makubaliano ya pamoja ya uchumi jijini Istanbul
trtafrika.com/swahili/articl…
128
Gavana mstaafu wa kaunti ya Migori nchini Kenya Okoth Obado amehukumiwa miaka 25 gerezani kwa mauaji ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu Sharon Otieno mwaka 2018.
Mahakama pia ilimhukumu msaidizi wa Obado wa zamani, Michael Juma Oyamo, miaka 25 jela huku aliyekuwa Karani wa kaunti hiyo Caspal Ajwang Obiero, akifungwa miaka 18.
Obado na wasaidizi wake wawili wa zamani walipatikana na hatia ya kumuua ya Sharon ambaye alikuwa na ujauzito wa miezi saba tarehe 23 Julai 2026.
167














