Greenjm retweeted
🚨EXCLUSIVE
Wale ambao hamkuweza kufika Mahakamani November 6, 2026 na mlitamani kumsikia Mhe. Lissu wakati anawashona Majaji kabla hawajasoma “Hukumu waliyopewa”.
Nimewaletea full clip ya Dakika 56 za Mhe. Lissu aisee ni noma na nusu.🙌
Repost 200
#FreeTunduLissu
Greenjm retweeted
Baba Yetu uliye mbinguni. Jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
Utupe leo Mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu. Kama nasi tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi. Lakini utuopoe maovuni, Amina🙏
Greenjm retweeted
A season for the history books 📖
@manutd's Bruno Fernandes is @EASPORTSFC Player of the Season ❤️
Greenjm retweeted
RATIBA YA KWARESMA 2026 ✝️
• Jumatano ya Majivu – Feb 18: mwanzo wa toba na unyenyekevu
• Dominika za Kwaresma – Feb 22–Machi 22: safari ya sala, kufunga na matendo ya upendo
• Dominika ya Laetare – Machi 15: furaha katikati ya toba
• Dominika ya Matawi – Machi 29: kuingia kwa Yesu Yerusalemu
• Alhamisi Kuu – Aprili 2: Ekaristi na Ukuhani
• Ijumaa Kuu – Aprili 3: mateso na kifo cha Kristo
• Mkesha wa Pasaka – Aprili 4: ushindi wa nuru
• Pasaka – Aprili 5: ufufuko wa Bwana 🙏✝️l
Greenjm retweeted
Leo tarehe 30 Desemba 2025, Mimi, Wakili Mzee Mpale Mpoki, na Wakili Hekima Mwasipu tulikwenda kumuona Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Antiphas Lissu, katika Gereza la Ukonga. Yu katika hali ya afya nzuri kiasi kwani kiwango chake cha sukari kwenye damu kimeongezeka kiasi ila Daktari amemuhakikisha kuwa kitadhibitika na kurudi hali ya awali kwa kuendelea kutumia dawa na Chakula.
Ametueleza kuwa amepokea barua kutoka kwa Naibu Msajili wa Mhakama Kuu ya Tanzania kuwa kesi yake itapangwa katika kikao maalumu cha Mahakama. Hata hivyo ikumbukwe kuwa sasa Mahakama Kuu ipo likizo hadi tarehe 31 Januari 2026.
Mwenyekiti Lissu amesisitiza kuwa uhaini ni kosa pekee lililotajwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ya Mwaka 1977 na hivyo halitakiwi kuendeshwa na kushitakiwa kwa utaratibu wa makosa mengine ya jinai.
Tutafikisha maelezo haya kwa uongozi wa Mahakama.
Vinginevyo amesema watu wawe imara na kuwa ATARUDI NA KUWA NASI.
Greenjm retweeted
Mungu ni Mwema siku ya leo tumefanikiwa kupata dhamana za ndugu zetu 4, wameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa kwa zaidi ya siku 20 katika kituo cha Polisi Chang'ombe. Lucy Simon Shayo ni kati ya watu ambao wamedhaminiwa Leo. Shukrani kwa Mawakili wetu kwa kazi kubwa .
Greenjm retweeted
WANANGU NAOMBA COMMENTS ZA #D9 ZA KUTOSHA.
WOTE TUNAELEKEA BUNGENI TIKTOK KUMSIKILIZA HABIL LEO ALISEMA ANA NONDO ZA MOTO SANA.
MWAGA MOTO WA KUTOSHA KUTUMA SALAMU KWA WAKOLONI WEUSI KUWA DISEMBA 9 TUTAKUWEPO🔥🔥
REPOST 500
#D9
#TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Greenjm retweeted
Jana nilipata nafasi ya Kuzungumza na Watanzania zaidi ya ELFU KUMI kwenye Bunge la wananchi lililokuwa Live TIKTOK, Instagram, Facebook na X.
Nilifurahi kusikia maoni Tofauti ya watanzania wenzangu, lakini pia kuna Maswali niliulizwa mimi binafsi na kuna pongezi pia nilipewa mimi binafsi NASHUKURU kwa haya yote.
Kuna Dada mmoja Alitoa maoni kutoka Instagram sikumbuki Jina lake vizuri ila sauti yake ipo bado kichwani mwangu hakuniuliza Swali alinipongeza na mimi kulingana na muda wa kuhutubia sikuweza kumjibu.
Nichukue nafasi hii adhimu kumjibu japo ni pongezi ambazo hazihitaji majibu. Alisema hivi “Sativa hongera kwa kazi nzuri unayofanya, wewe ndio umekuwa Sababu kubwa ya vijana kufuatilia SIASA, naomba usije ukawaangusha VIJANA WENZIO huku mtaani. Vijana wanakupenda sana na wanakufuatilia sana.”
Alikuwa akiongea haya akiwa na furaha lakini kama anatetemeka, kisaikolojia naweza kuitafsiri kama hakuwahi kufikiri kama siku moja ataongea kitu mimi nikakisikia moja kwa moja kutoka kwake, hivyo kuongea mbele yangu vile aliona kama ngekewa na bila shaka huyu ni FAMILIA SANA.
MAJIBU YANGU.
Kwanza Popote ulipo Sista naomba nikuambie machache kutoka kwangu ambayo najua unayajua ila nataka nikuhakikishie.
1. Mimi SATIVA ni zao la watanzania, Nilitekwa kwa siku 4 waliopambania nipatikane ni WATANZANIA. Mitandao ili simama siku zote hizo kunitafuta.
2. Mimi SATIVA nina kovu la risasi ya kichwa, waliokuwa wa kwanza kunitibu ni Watanzania kwa michango yao kutoka kila kona ya nchi.
3. Mimi SATIVA sina Bei kwenye hizi harakati. Na wao wanajua misimamo yangu. Hilo la kuwasaliti watanzania sahau.
Hayo mambo matatu ndio sababu ya Mimi SATIVA kuwa upande wa watanzania kila siku na hata milele. Siku pekee ambayo sitakuwa upande wa watanzania basi ni KIFO.
Nashukuru kwa Upendo na hii meseji ifike kwa vijana wote ambao wananiamini kwenye mapambano haya na wapo na mimi kwenye kila hatua. Tutashinda pamoja wanangu kuna wakati unachoka kama mwanadamu ila nikikumbuka mliyofanya kwangu nasimama na kuendelea na safari ya UKOMBOZI.
SATIVA
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Greenjm retweeted
🚨 BREAKING: Bunge la Ulaya limepitisha AZIMIO kali sana dhidi ya serikali ya Tanzania (27 Nov 2025)
🔨Linakemea mauaji ya siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi, makaburi ya HALAIKI na VIBURI vya jeshi lapolisi.
🔨Linamtaja moja kwa moja Tundu Lissu na kulaani kesi yake ya uhaini (Kesi ya MCHONGO).
🔨Linaitaja serikali kusitisha ukandamizaji na kumwachia Tundu Lissu MARA MOJA.
🔨Linadai uchunguzi wa kimataifa unahitajika.
🔨Linaagiza EU (Umoja wa ULAYA) kusitisha misaada ya moja kwa moja kwa serikali na kufikiria kuweka vikwazo dhidi ya serikali ya TANZANIA.
Hii si azimio la kawaida — ni pigo kubwa sana kwa serikali.
Kesho MAAZIMIO HAYA YANAPIGIWA KURA KUPITISHWA NA KUWA MSIMAMO RASMI WA UMOJA WA ULAYA.🙌🏿
REPOST 500
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Greenjm retweeted
"Si chombo huru, na hakiwezi kutoa ukweli wala haki katika mazingira ambapo serikali ndiyo mtuhumiwa mkuu." Mhe. @HecheJohn
Greenjm retweeted
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 147
Anaendelea Mhe. Lissu
Waheshimiwa Majaji,
Hoja yangu ya pili ni kwamba, huyo shahidi ni shahidi wa namna gani?
Kwa mujibu wa kanuni ya 3 lazima awe yuko chini ya amri ya ulinzi.
Sasa Mahakama hii inawezaje kujua shahidi kama yuko chini ya amri ya ulinzi?
Naomba kuwarejesha kwenye Kanuni ya 5(1) ambayo inasema mtu huyo lazima awe amebainishwa katika maombi.
Maana ya haya maneno ni nini?
Maana yake rahisi ni kwamba mtu ambaye jina lake lilipelekwa kwa jaji likaombewa ulinzi.
Jaji awe anamfahamu kwa jina na kuwa maisha yake yako hatarini.
Naomba niwarejeshe kwenye hati ya maombi ya tarehe 14 Julai 2025, hiyo application ina viapo viwili, ina kiapo cha SSA Mose Kaima na ACP Amini Mahamba.
Waheshimiwa majaji kwenye hiyo hati ya maombi, hivyo viapo viwili hakuna kiapo hata kimoja chenye jina la shahidi hata mmoja.
Katika orodha ya mashahidi wanaoitwa wamepewa ulinzi, hakuna hata jina moja la shahidi ambalo lilipelekwa kwa Jaji Mtembwa.
Hiyo amri ilitolewa on insufficient ground na ilitolewa kwa concealment (kwa kuficha Ushahidi kwa mahakama) na mawakili wa serikali.
Walipaswa kupeleka majina kwa jaji lakini hawakufanya hivyo, hivyo Jaji Mtembwa hawafahamu na nyie waheshimiwa majaji hamuwafahamu, wanajulikana tu na waliowaleta, hivyo sitaki kusema kuwa amri ya ulinzi ilipatikana kwa fraud but by concealment by the State Attorneys.
Waheshimiwa majaji kama hiyo ni haki then tunahitaji tafsiri mpya ya haki huku Duniani.
Waheshimiwa majaji sio tu kuwa hakuna majina ya mashahidi ila hakuna hata majina ya wanaowatishia ni maneno tu, maneno matupu kabisa.
Hata nature ya vitisho haijaelezwa kwamba wanatishiwaje, kivipi na nani anawatisha? Haipo kabisa.
Waheshimiwa majaji, sasa niende kwenye hoja yangu ya tatu ambayo ni kuhusu amri ya Mahakama Kuu;
Mahakama kuu ilitoa ulinzi upi? Ili kujibu hilo swali sawasawa naomba nitangulize kanuni ya 7(1) ya Kanuni za Ulinzi wa Mashahidi.
Kanuni inasema kwamba hatua za ulinzi wa shahidi zitadumu kwa kipindi cha usikilizwaji wa kesi isipokuwa kama amri husika itaashiria vinginevyo.
Kwenye uamuzi wa Jaji Mtembwa maombi ya Jamhuri yalikuwa kutokuonyesha utambulisho wa mashahidi wanaotarajiwa kwa kutokuweka wazi nyaraka zinazoweza kupelekea shahidi kujulikana, matumizi ya majina bandia, amri nyingine yoyote kwaajili ya usalama wa mashahidi wa Jamhuri wakati wa mwenendo wa ukabidhi au wakati wa kesi kusikilizwa.
Naomba waheshimiwa majaji pia muangalie kanuni ya 6(1) ili muone ni maombi gani mengine ambayo kama upande wa mashtaka wangetaka wangeyaomba.
Kanuni hii imetaja orodha ya amri zinazoweza kuombwa na kutolewa na mahakama. Zimeelezwa kwa uwazi kabisa kwenye kanuni husika hii itatusaidia kuelewa ninachotaka kukisema.
Waheshimiwa majaji, katika kanuni hiyo ya 6 kuna amri 16 ambazo zinaweza kuombwa na hiyo ya kutumia kizimba maalumu hawakuomba mawakili wa serikali.
Katika dunia hii waheshimiwa majaji, usipoomba hupewi, hili sio takwa la kisheria tu ni takwa pia la kibiblia kuwa ombeni nanyi mtapewa.
Jamhuri walipewa amri nne walizoomba lakini amri ya kutumia kizimba maalum hawakuomba, hivyo hawawezi kupewa kitu ambacho hawakuomba katika lugha ya kisheria, they are estopped.
Waheshimiwa majaji kwa maoni yangu kanuni hizi zilitungwa kuwafurahisha waendesha mashtaka na watu wao. They are totally one sided.
Waheshimiwa majaji kwa mujibu pia wa kanuni ya 8 kama Jamhuri wangeona amri za Jaji Mtembwa haikulinda mashahidi sawa sawa walikuwa na fursa ya kuleta maombi mbele yenu kwa mfano kuwa tunaomba kutumia kizimba maalum, hawajaleta maombi hayo.
Now it is late in the day to sneek in today kuleta hao mashahidi. Wameleta wakijua kanuni hizi hamtazisoma au mshtakiwa atanyamaza. Wamelalia haki yao, waachwe waendelee kuilalia.
Part 148 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.



































