
Don't see others doing better than you, Beat your own records everyday because, Success is a fight between YOU & YOURSELF #FeelTheDiffelence
Joined December 2014
- Tweets81.9K
- Following363
- Followers1.2K
- Likes11K
BekaBOY 0.2 retweeted
Daaah Jamaa ame yaishi Maneno Yake🥹🙏🏽🙇🏽♂️
MUNGU AMLINDE
Repost 100 tu🤌🏾
#FreeTwahaMwaipaya 🙌🏾
BekaBOY 0.2 retweeted
Kwa ajili ya Tundu Lissu, hawa washirika wa madhulmati wote tuwakatae
Una sababu gani za kutumia bidhaa za hawa watu ?
BekaBOY 0.2 retweeted
Tuanze hapa
Mgomo wa bidhaa/huduma unaanza rasmi kwa wale viongozi wote wa ccm/machawa/na wauwaji wanaouza bidhaa au kutoa huduma kupitia biashara zao.Kama wewe ni Mtanganyika unaependa haki anza kugomea hizo bidhaa ambao zina . Mfano mimi kuanzia leo nyumbani kwangu ni marufuku kununua Mtungi wa Taifa gesi na Sitopanda basi la Abood
@MariaSTsehai
@lifeofmshaba
@AdvocateMaria92
@EliasariaII
@SautiWatanzania
@Liberatus80
@Nuruvazi01
@Tanzaiite
@CuteMaria26
@2twelve4
BekaBOY 0.2 retweeted
Hii fursa tunapaswa kuitumia vizuri sana
#NoJusticeNoAFCON
BekaBOY 0.2 retweeted
Fursa imeongezeka! Lazima maandamano ya AFCON iwe kubwa kama makao makuu yatakuwa 🇹🇿👊🏽
#NoJusticeNoAFCON
BekaBOY 0.2 retweeted
Replying to @akilichache
Ukianza kujenga uhusiano mzuri na Mungu huwezi kupinga ndoa, watu wamjue Mungu kwanza kabla ya kukimbilia kupinga na kukataa ndoa.
BekaBOY 0.2 retweeted
“Today the High Court has confirmed what we have said from day one: the treason charge was a political fabrication. The prosecution failed to prove any intention to intimidate the government.
Instead of ordering my release after 577 days in detention, the court has convicted me of an offence I was never charged with and never given a chance to defend.
This is not justice. This is damage control.
History will record how the court searched for a lesser charge simply to keep me in prison.” Tundu Antipas Lissu
November 6, 2027
—Admin.
BekaBOY 0.2 retweeted
Wakati Lissu anafanya mitigation alianza kwa kusema;
“Historia haijawahi kuwa nzuri kwa Majaji wanaowaonea wasio na hatia”
na akamaliza kwa kusema “Mimi siombi msamaha kwa kuwa sio mkosaji, kwa sasa nimemaliza, toeni huo uamuzi mlioelekezwa” 💪🏿💪🏿💪🏿
BekaBOY 0.2 retweeted
“Waheshimiwa Majaji, naomba nimalizie. Uamuzi wa kunitia hatiani kwa kosa ambalo sikushitakiwa nalo, na ambalo sikupata fursa ya kujitetea dhidi yake, kwa lengo la kubalansisha tu, una athari kubwa. Athari yake ni kwamba mmewapa kinga wale waliohusika na mauaji, kwa sababu watasema kwamba wale waliochochea wamekutwa na hatia. You are covering mass murderers. Serikali hii imeua watu wengi kuliko serikali zote zilizowahi kutawala nchi hii. Mara ya mwisho mauaji ya halaiki kutokea kwa kiwango hiki ilikuwa wakati wa Vita vya Majimaji. Mmewapa sababu ya kusema kwamba mkosaji aliyesababisha mauaji hayo amekutwa na hatia. Kama mnafikiria kwamba uamuzi huu utawasaidia, hautawasaidia. Watawajibishwa mahali pengine. Serikali ya Nyerere iliua watu 37. Wakati huo, Mwinyi alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na alijiuzulu. Shahidi alikuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na alijiuzulu. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Peter, naye alijiuzulu. Leo hii, serikali imeua watu ambao idadi yao, kwa makadirio ya chini kabisa, ni 500, lakini hakuna aliyejiuzulu. Uamuzi wenu hautaficha ukweli huo. Nimewakumbusha, Waheshimiwa Majaji, kwamba katika Sentencing Guidelines, kipengele cha kwanza kinaelekeza kwamba adhabu ya faini itolewe isipokuwa pale ambapo kosa ni kubwa. Uchochezi, ambao sikushitakiwa nao, hauna adhabu maalumu. Ndiyo maana Wakili Mkuu wa Serikali anakwenda kwenye General Provisions. Waheshimiwa Majaji, namalizia kwa kusema: TOENI HUKUMU AMBAYO MNAYO, AMBAYO MMEAGIZWA KUITOA.”
Tundu Antiphas Mughwai Lissu, 6 Novemba 2026, Mahakama Kuu ya Tanzania, katika hukumu ya kesi yake ya uhaini.
BekaBOY 0.2 retweeted
Mimi sio mtu wa emotions sana ila leo niko very emotional, I hope tutapewa dhamana au tutapewa fine, binafsi niko tayari kulipa hata yote peke yangu, I hope TAL atarudi nyumbani leo inshAllah.
BekaBOY 0.2 retweeted
TUNDU LISSU ; Waheshimiwa Majaji toeni hukumu ambayo mnayo. TOENI HUKUMU AMBAYO MMEAGIZAWA. Nimemaliza . Asante.
BekaBOY 0.2 retweeted
“Waheshimiwa Majaji nashukuru kwa fursa ya kuzungumza. Naomba mnisikilize kwa makini kama ambavyo mmenisikiliza kwa makini mwaka mzima. Naomba pia m’rekodi proceedings kama mlivyo’rekodi vizuri mwaka mzima na nusu. Leo Waheshimiwa majaji ni siku ya 577 nikiwa gerezani kwa kosa la uhaini. Ndiyo kosa kubwa Kuliko yote katika Jamhuri ya Muungano. Ndiyo kosa pekee lililotamkwa katika katiba, kosa la uhaini. Kwa siku 577 nimeitwa mhaini. Kosa ambalo kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) ambapo adhabu yake inaeeza kuwa ni KIFO. Baada ya siku 577 baaada ya wingu jeusi la adhabu ya kifo kuning’inia juu ya kichwa changu. Leo Waheshimiwa Majaji mmeniita MCHOCHEZI. Kosa ambalo wala halijapangiwa adhabu. Unaona hapa, wakili mkuu wa serikali anahangaika kutafuta hii adhabu yake ni nini., anasema nipewe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine, nihukumiwe kifungo cha miaka mitano gerezani. Hii maana yake ni nini Waheshimiwa Majaji? Waheshimiwa majaji mmesema wenyewe hakukuwa kosa. Kwa hiyo nimekaa gerezani siku 577 bila kosa lolote. Kuna kitu kimoja hamjakisema nitakisema kwa ajili ya kumbukumbu za Mahakama. Ushahidi wangu umethibitisha kwamba hii ilikuwa kesi ya kisiasa. Kugeuza Mahakama kuwa uwanja wa mapambano ya kisiasa, it’s an obvious political persecution. Kwa sababu ni political persecution inabidi vi’sababu vitangenezwe vya kumfunga huyu mgomvi wetu. Vi’sababu vya kumfunga huyu mpinzani wetu. Hili kosa la UCHOCHEZI ni kisa ambalo ninyi Waheshimiwa Majaji mmelitengeneza. Mimi nilishitakiwa kwa UHAINI na kusambaza taarifa za uongo. Mmetafuta kosa ambalo halikuwepo, mmenipa. With all due respect mmefanya hivyo kwa sababu za kisiasa na kwa maelekezo ya kisiasa tu. Ni kama mmeambiwa, huyu mtu hana kosa lakini tafuteni kosa lingine dogo, isije ikaonekana serikali imepata aibu. Mimi ninajua mtani’hukumu. Na mnaonekana tayari mnayo hukumu, l feel it in my heart.”
Tundu Antiphas Mughwai Lissu, O6 November 2026, Mahakama Kuu ya Tanzania katika hukumu ya kesi yake ya uhaini.


























