KIJANA MWEUPE retweeted
Ila wadada wana kazi sana just imagine mtu kataka tucheze 654321 sijui,nimejibu imekuwa kesiii 😂😂😂😂💔💔🙌🏼
KIJANA MWEUPE retweeted
#MICHEZO: Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika CAF limeipitisha Lugha ya Kiswahili kama Lugha rasmi ya kwenye shughuli zote za soka barani Afrika.Uamuzi huo wa kihistoria umefikiwa leo Jumamosi, Novemba 21, 2026, katika Mkutano Mkuu wa 48 wa CAF unaofanyika mjini Abuja, Nigeria
Pendekezo la kufanya marekebisho kwenye katiba na kanuni za CAF (Kifungu cha 3 ibara ya 1, 2, na 3 pamoja na Kifungu cha 7 cha Kanuni za Mkutano Mkuu) liliwasilishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) chini ya Rais wake Wallace Karia.
Hoja hiyo ya Tanzania iliungwa mkono kikamilifu na mashirikisho ya soka ya Kenya (FKF) na Uganda (FUFA), ikiwa ni sehemu ya maandalizi na ushirikiano wa ukanda wa Afrika Mashariki kuelekea mashindano ya AFCON 2027 yatakayoandaliwa kwa pamoja na nchi hizo tatu.
Kwa uidhinishwaji huu, Kiswahili sasa kinaungana na lugha nyingine kuu zilizokuwa zikitumiwa na CAF (kama vile Kiingereza, Kifaransa, na Kiarabu) katika mawasiliano rasmi, nyaraka, mikutano mikuu, pamoja na mikutano ya waandishi wa habari kwenye mashindano ya CAF.
✍: @nickymeena_
#Michezo #Hainakuchoka #EastAfricaTV







